Msururu ya utekaji nyara ukiendelea kushuhudiwa nchini, chama kinachotetea haki ya kibinadamu{KHRC} kimewasuta baadhi ya viongozi serikalini kikiwataka kujiuzulu kutokana na matamshi yao yanayodhaniwa kutojali utekaji nyara ambao umesuhudiwa nchini tangu maandamano ya vijana ya mwezi wa sita mwka uliopta.
Shinikizo hili linajiri baada ya baadhi ya vijana waliotekwa nyara kuachiliwa. KLHRC ilitaja baadhi ya majina ya viongozi ambao waliwataka kujiuzulu kutokana na matamshi waliotoa wakati taifa lilikumbwa na wimbi la utekaji nyara kwa vijana.
Baadhi ya majina ya viongozi waliotajwa na tume hiyo ni pamoja na naibu rais Kithure Kindiki, waziri wa mambo ya ndani Kipchumba Murkomen, kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung'wah, spika wa seneti Amason Kingi, mbunge wa Kapseret Oscar Sudi, mbunge wa Sirisia John Waluke na mbunge wa Tiaty William Kamket kuhusu matamshi yao katika wakati tete ambapo Wakenya wanatafuta majibu juu ya utekaji nyara unaotekelezwa.
Wakati huo, KHRC inamtaka inspekta jenerali wa polisi, Douglas Kanja kuwasilisha ombi la kujiuzulu baada ya utekaji nyara huo kutokea chini ya ulinzi wake.
Kulingana na tume hiyo, maoni yanayotolewa na wanasiasa hao
yanakiuka utawala wa sheria na nyadhifa za uongozi wanazoshikilia.
Tume hiyo inayotetea haki za kibinadamu inataka uchunguzi usio na upendeleo na wa kina kufanywa kuhusu kauli wanazozitoa kuhusiana na visa vya vijana wanaowajibisha serikali kutekwa nyara.
KHRC imeshauri kuwa viongozi watakaopatikana na hatia wawajibishwe kwenye asasi husika pamoja na kuzuiwa kushikilia nyadhfa za umma. .