Moja wapo wa vijana walioachiliwa Jumamosi baada ya kudaiwa kutekwa nyara kwa takribani wiki mbili amezungmza kuhusu alivyotekwa na kuzuiliwa. Billy Mwangi kutoka Embu amezungumza kuhusu kutekwa nyara kwake akielelzea baadhi ya matukio aliyopitia.
Akizungumza kwenye mahojiano na mtengenezaji wa mmoja wa maudhui nchini Kenya, Billy amesema kwamba alitekwa nyara wakati akisubiri kinyozi wake kumnyoa Jumamosi aliyotekwa nyara mwendo wa saa tisa adhuhuri.
Mwangi amesema kwamba alifika kweny kinyozi na kupata laini ndefu ya wateja waliokuwa wakishughulikiwa ana akaamua kusubiria kwa muda wa angalau dakika 15 hadi 20 ili afikiwe ndio anyolewe. Kwa mujibu wake, amesema kwamba yeye ni Mkiristo na hupenda kushiriki ibaada kila Jumapili akiwa nadhifu.
Kwenye maelezo yake. Akiwa akisubiri wateja waliokuwa mbele yake kunyolewa gari aina ya pick-up double cabin ya raptor ya rangi nyeupe lilifika kinyozini pale na watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao kushuka na kumbeba hobela hobela hadi kwenye gari hilo liliondoka naye bila ya kusaidiwa na watu waliokuwa kinyozini pale.
“Walinichukua tu ju juu hata sikumbuki mtu yeyote akisema msimchukue msimchukue.” Alisema Biily Mwangi.
Wakati huo, Billy amesema kwamba alifunikwa uso na kutokea hapo hakujua wala kufahamu alikokuwa anapelekwa.
Baada ya kuachiliwa, kijana huyo ambaye sehemu kubwa ya Wakenya kupitia mitandao ya kijamii na heshitagi walitaka kuachiliwa kwake , amewashukuru wote waliochangia kwa njia moja au nyingine ikiwemo baba wake kwa kutetea kuachiliwa kwake.
Aliporudi nyumbani kwao Jumamosi asubuhi mwendo wa saa mbili, Billy alikuwa amenyolewa licha ya kuwa alitekwa nyara kabla ya kunyolewa.
“Tulinyolewa! Binafsi nilinyolewa na sijui ni lini nilinyolewa lakini nilinyolewa. Nilichanganyikiwa. Sijui chochote, niliogopa na kuchanganyikiwa.” Alisema Billy kwenye mahojiano hayo.
Hata hivyo, Billy amesema hakumbuki chochote kilichokuwa kinatukia wakati alikuwa ametekwa nyara. Amesema kwamba hakufahamu wakati dunia ilikuwa inaadhimisha mwaka mpya wala kujua ikiwa alikuwa katika mwaka wa 2025 au la.
Kijana huyo aliachiliwa pamoja na vijana wengine wanne
kutoka sehemu mbali mbali, alisema kwamba alijipata akiwa Nyeri mjini na hapo
ndipo ndipo aliabiri matatu yenye maandishi ya Embu na kuelekea nyumbani.