Wakaazi wenye hasira na ghadhabu waliamua kuchukua sheria mkononi kwa kuupelekwa mwili wa msichana anayedaiwa kuuliwa kwenye boma la mshukiwa wa mauaji ya marehemu na kkuacha mlangoni pa mshukiwa huyo.
Kisa hicho cha Jumatano mchana kilishudia wakaazi wenye hasira wakishambulia maboma mawili ya washukiwa katika eneo la Mahigaini na Gushue katika kaunti ndogo ya Mwea Mashariki.
Kwa mujibu wa taarifa, mwili wa msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 ulipatikana asubuhi ya Krisimasi karibu na mto Thiba katika kaunti ndogo jirani ya Mwea Magharibi.
Katika kisa hicho, polisi walilazimika kutumia vitoa machozi kusambaratisha umma uliokuwa na hasira walipopelekwa mwili wa msichana huyo ukiwa jenezani kwenye boma la mshukiwa mmoja.
Ghadhabu za wanakijiji zilielekezwa kwa familia ya mshukiwa huyo zikiitaka mamlaka kuhakikisha familia ya mshukiwa inafurushwa kutoka kwa kijiji hicho. Wanakijiji wanadai kuwa jamaa wa familia hiyo alihusika katika mauti ya marehemu.
”Hii familia pia kama watu wa hii kijiji mnaomba tutafanya hivi si mnataka haki.”
“Familia ya mwenye amefanya hii kitendo wote wahame.”
Sauti za wakaazi wenye hasira walisikika
wakilalama