logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DCI yamtaka waziri Justin Muturi kuandikisha taarifa kuhusu madai ya kutekwa nyara kwa mwanawe

Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imemwita waziri wa utumishi wa umma, utendaji na usimamizi wa uwasilishaji Justin Muturi

image
na OTIENO TONNY

Yanayojiri13 January 2025 - 11:15

Muhtasari


  • Idara hiyo vilevile ilisema kuwa baadhi ya makesi za utekaji nyara zilizoripotiwa polisi zinachunguzwa na sasa ziko mahakamani.
  •  Waziri huyo wa utumishi wa umma ameonekana kutofautiana kimaoni na na maafisa kadhaa wa serikali. 



Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imemuita waziri wa utumishi wa umma, utendaji na usimamizi wa uwasilishaji Justin Muturi.

Waziri huyo anahitajika kurekodi taarifa kama sehemu ya kusaidia katika uchunguzi unaoendelea kuhusu kutekwa nyara kwa mwanawe mwaka jana na kuhusu hotuba aliyotoa kuhusiana na utekaji nyara unaoendelea nchini.

Zaidi ya hayo, idara hiyo ilikubali matamshi ya Muturi hadharani ya kufadhaika kuhusu kasi na matokeo ya uchunguzi wa kesi za utekaji nyara kote nchini.

Idara hiyo ilifichua kuwa ni mtoto wa waziri Muturi pekee ambaye kufikia sasa ameandika taarifa kuhusu kutekwa nyara kwake, na ushirikiano zaidi ulihitajika kuendeleza kesi hiyo ikiwemo baba taarifa kutoka kwa baba yake.

‘’Kesi ya madai ya kutekwa nyara inayomhusisha mwanawe Waziri Justin Muturi iko mbele ya idara ya upelelezi wa makosa ya jinai Kilimani. Ikizingatiwa kuwa ni mtoto pekee aliyejitolea kurekodi taarifa, tunataka kumwalika waziri  Muturi na mtu mwingine yeyote aliye na habari kuhusu tukio hilo kurekodi taarifa na DCI Kilimani,” Hii ni kutokana na ujumbe kutoka kwa idfara ya upelelezi.

Idara hiyo vilevile ilisema kuwa baadhi ya makesi za utekaji nyara zilizoripotiwa polisi zinachunguzwa na sasa ziko mahakamani na hata kesi za sasa hivi za utekaji nyara hazitaachwa nyuma .

Akizungumza awali jumapili 12, Januari 2025, wakati wa kikao na wanahabari Jumapili, Muturi alisema Kenya ni nchi ya kidemokrasia na kila mtu yuko huru kueleza masuala yake bila woga.

Waziri huyo wa utumishi wa umma ameonekana kutofautiana kimaoni na na maafisa kadhaa wa serikali na kusema kwamba vijana wa Kenya wanapaswa kuruhusiwa kutoas maoni yao kwa uhuru  bila kutishwa na mtu yeyote.

‘’ Ni jukumu letu kama serikali kuhakikisha kuwa kila mtu anaishi kwa njia huru hii ikiwa ni kusema kile mtu anafikiria ata kama ni nkusema kuwa hawanitaki, hiyo ni maoni,’’ Alisema Muturi.

Mwanasheria mkuu  huyo wa zamani alisema ni makosa kwa serikali kudai kuwa haihusiki na utekaji nyara lakini kwa upande mwingine inashindwa kueleza nani alikuwa nyuma ya utekaji huo.

‘’Jukumu kuu la serikali  ni kulinda maisha na riziki ya raia wake na haiwezi kudai kuwa haitambui ukiukaji mkubwa wa haki za Wakenya za kuishi bila kufungwa kwa njia isiyo halali na ukiukwaji wa haki yao ya kuishi isiyoweza kuondolewa. ” Alisema Muturi.

Muturi alisema kuwa ana wasiwasi hasa kuhusu mwanawe ambaye alitekwa nyara miezi misita iliyopita na kuachiliwa baadaye na waliomteka nyara,  wakati huo Muturi akihuduma kama mwanasheria mkuu nchini na mpaka mwaka wa 2025 hakuna hata mtu mmoja ambaye ameshikwa na polisi kwa madai ya utekaji huo.

"Mimi binafsi nimeteseka kwani mwanangu alitekwa nyara na kutoweka, sikuwa na uhakika kama yu hai au amekufa, jambo lililotufanya tuingiwe na wasiwasi na kuniacha mimi, mke wangu na familia yangu katika hali ya taharuki. Sikuweza kumtafuta mwanangu licha ya kufanya maombi na matakwa kadhaa kwa ngazi zote za vyombo vya usalama." Aliongezea Muturi.

Hii inakuja ikiwa taifa la Kenya linakumbwa na msururu wa  utekaji nyara wa vijana hasa wale ambao wanadaiwa kutumia mitandao ya kijamii kuikosoa serikali kwa njia isiyofaa. Kufikia sasa bado kuna baadhi ya familia ambazo hazijafanikiwa kujua waliko wapendwa wao ambao wana amini walitekwa nyara.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved