Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko alikutana na aliyekuwa naibu wake Polycarp Igathe katika mtaa wa Runda Nairobi.
Wawili hao walikutana kwenye sherehe ya kuajindaa kwa harusi ya kitamaduni ya
mwanawe Polycarp Igathe, Matilda Igathe na mchumba wake Luios Muihengi Kimanzi.
Sherehe hizo ziliwaleta pamoja ndugu, jamaa pamoja na marafiki wakiwemo vigogo mashuhuri kutoka sehemu tofautitofauti.
Sonko ambaye anajulikana kuwa na uwezo wa kununua mivinyo za bei ghali alimuzawadi Polycarp Igathe na pombe aina Johnnie Walker King George V edition inayogharimu thamani ya Ksh 76,000 kwa chupa moja.
Akipokea zawadi hiyo Igathe alimushukuru Sonko akisema “ hii pombe ya walker king imeletwa na bosi wangu , Gavana wangu sonkoree. Sasa wewe ni rafiki yangu , umekuja na familia ya kimani umekua mkoo, tukikutaa uko inje wewe ndo unalipa bill.