Askofu
mmoja katika kaunti ya Homabay amewashangaza wenyeji baada ya kufumaniwa akishiriki mapenzi na bintiye..
Maafisa wa usalama kutoka kaunti ndogo ya Rangwe wanamzuilia mwanaume huyo kwa kosa la kuhusika kwenye mapenzi na mwanawe wa damu.
Maafisa walipata habari kutoka kwa maafisa wenzao wa kituo cha Ndiru baada ya kupashwa habari na wanakijiji.
Kulingana na walioshuhudia, askofu alifumaniwa na mwanakijiji mmoja akiwa katika tendo na mwanawe ambaye ni mama wa watoto watatu.
Msimamizi wa kituo cha polisi cha Rangwe Magdaline Chebet alisema kwamba walipata habari kutoka kwa wanakijiji walioshangazwa na tabia za mmoja wao baada ya kumfumania akiwa kwenye tendo la ndoa na mwanawe ambaye alikuwa ameaoleka hapo awali na baadaye wakatengana na aliyekuwa mumewe.
Shinkizo za wanakijiji ziliwafanya maafisa wa polisi wa kituo hicho cha Ndiru, wakiongozwa na mkubwa wa kituo hicho kumtafuta mshukiwa na kumkamata.
Askofu alikamatwa nyumbani kwake pamoja na mwanawe.
Kwa sasa mshukiwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Ndiru huku uchunguzi zaidi ukiendelezwa na maafisa wa usalama
Bintiye askofu, alipelekwa hospitalini, baadaye akahojiwa na kuachiliwa kurudi nyumbani.