Papa
Francis alianguka na kujeruhiwa mkono wake wa kulia siku ya Alhamisi.
Katika taarifa, ofisi ya mawasiliano ya Vatican ilisema kwamba kutokana na kuanguka Alhamisi asubuhi katika Casa Santa Marta, makazi ya papa, papa huyo mwenye umri wa miaka 88 alipata mchubuko kwenye mkono wake wa kulia.
Hata hivyo, kwa bahati nzuri, mkono wake hauvunjika.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa mkono wake umetulizwa kama hatua ya tahadhari.
Picha rasmi za Alhamisi zilionyesha papa akiwa amefunga mkono wake kwa kombeo la kitambaa alipokuwa akifanya mikutano.
Licha ya ajali hilo, Francis alifanya mikutano mitano siku ya Alhamisi kwa mujibu wa Vatican, ikiwa ni pamoja na Alvaro Lario, Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, na mapadre kutoka chuo cha Argentina kilichoko mjini Roma.
Siku ya Jumatano, papa aliongoza hadhira yake kwa ujumla mjini Vatican na alionekana mwenye roho nzuri, akimrushia mbwa mpira wa tenisi wakati wa maonyesho ya sarakasi.
Papa amekumbwa na matatizo kadhaa ya kiafya katika miaka ya hivi majuzi na hii ni mara ya pili ambapo anaanguka katika kipindi cha wiki chache.
Mapema Desemba, alionekana na jeraha kubwa kwenye kidevu chake baada ya kuanguka na kugonga meza yake ya kitanda wakati wa usiku.
Tangu 2022, papa amekuwa akitumia kiti cha magurudumu kutokana na matatizo ya uhamaji yanayosababishwa na maumivu kwenye goti lake.
Katika wasifu wake uliochapishwa hivi majuzi "Hope", Francis alisema kwamba yuko katika afya njema na alikataa kujiuzulu kutoka kwa wadhifa wake, lakini akasema kwamba "ukweli ni, kwa urahisi kabisa, kwamba mimi ni mzee."
Alisema "ilikuwa aibu mwanzoni kutumia kiti cha magurudumu, lakini uzee hauji wenyewe, na lazima ukubaliwe jinsi ulivyo."