Mwenye kiti wa chama cha wafanya kazi "COTU" Frances Atwoli ametofautiana vikali na aliyekua rais wa nne wa Jamuhuri y Kenya Uhuru Kenyatta. kwa kile kilchoonekana kama kumujibi rais huyo wa zamani kutokana na madai yake,ambayo watu wa upande wa serikali waliyachukulia kama uchochezi kwa vijana kupigana na serikali ilioko mamlakani.
Atwoli alizungumza alipokua ameandamana na rais William Ruto kwenye safari yake ya magharibi katika kaunti ya kakamega.
Msimamizi huyo wa chama cha wafanyi kazi alisema kuwa alikua amependekeza waangalie mashart ya rais anaestaafu, mienendo ambayo anafaa kuwa nayo lakini watu wakamnukuu visivyo na kudhani kuwa alitaka kuuongoza miaka ya rais kuwa mamlakani.
"Mwaka 2007 nilisema tuangalie katiba ili tumpe Masharti rais yeyote anayestaafu, watu wakasema eti nataka kuongeza hatamu ya rais kuwa mamlakani. haikuwa hivo." Atwoli alisema.
"Mtu anaamua kusema , vijana lindeni mali yenu, vijana wadogo wana mali gani ya kulinda, badala ya kusema nyinyi mnisaidie mali yangu isichukuliwe, yeye ana wasiwasi na mali yake." Atwoli aliongeza.
Rais Msitaafu alikua amewarai vijana kutetea haki yao na kulinda mali yao. uhuru alikuwa amewasisitizia vijana kutonyamaza wakati maali yao inaibiwa bali kujitokeza na kupigania haki yao kwani wao ndio tegemeo lililopo na kizazi cha baadaye.
Atwoli alizungumza wakati akiegemea upande wa kujibu maneno haya ya rais huyo wa zamani. wakati huo kiongozi huyo wa chama cha wafanyi kazi alionekana kuirai jamii ya mulembe kusimama na rais
Francis Atwoli aliteuliwa mara ya kwanza kama kama mwenyekiti wa cha cha wafanyakazi mwezi August 2001. amejulikana sana kwa kufanya kazi karibu sana na marais walioko mamlakani, akianza na rais mstaafu, Hayati Daniel Moi, Mwai Kibaki, rais mstaafu, uhuru kenyatta na rais William Ruto ambaye yuko mmlakani kwa sasa.
Francis Atwoli alikuwa Mwandani wa Uhuru kenyatta wakati akiwa bado rais, na hata kuhusika katika kampeni ya kumpigia debe Raila Odinga kwenye kura ya kuwania urais alipokuwa ameidinishwa na na Rais huyo mstaafu Uhuru Kenyatta.