Aliyekuwa Gavava wa Nairobi Mike Sonko amejitolea kumulea na kumukuza mtoto aliachwa yatima baada ya babake kuuliwa.
Marehemu alikutana na mauti yake asubuhi ya Jumatatu mwendo wa saa kumi na mbili alipokua akimsindikiza mwanawe wa miaka mitatu shuleni.
Kisaa hiki kilitokea katika mtaa wa Mathare jijini Nairobi.
"Nilisikia nduru, kutoka inje nikaona mtu amelala chini, kando yake mtoto mdogo akiwa amekaa chini huku akilia akisema saidieni babangu amedungwa kisu," jirani alisema.
Sonko ameonesha kusikitishwa na kitendo hicho cha kihuni cha binadamu wasio na utu. Ameomba uchunguzi wa kina kufanywa ili haki ipatikane.
"Hili nalo linauma, nimeumizwa sana na hadithi ya kijana mdogo ambaye babake alidungwa na kuuliwa na wanaoshukiwa kuwa majambazi katika mtaa wa Mathare 4A.
Baba alikua fundi wa ujenzi na mzazi wa kipekee. Hili linaonesha alivyojaribu kujituma kumulea mwanawe maana mtoto alikuwa tu wa miaka mitatu.
Kijana mdogo alilia huku akitizama babake akidungwana majambazi pasipo usaidizi wowote, inahuzunisha kwamba aliaga kabla ya ambulensi kufika," Sonko aliandika katika mtandao wake wa X.
"Kwenye tukio maafisa wa usalama walipata kijibakuli cha mtoto kikiwa na chakula cha mtoto wake. Ishara ya mzazi anayejituma kumulea mwanawe licha ya kuwa familia ya mzazi mmoja.
Kwa vile mtoto ameaacha yatima kama kawaida, ningependa aletwe kwangu, nitachukulia mahali babake ameaachia na kumukuza mtoto," aliongeza gavana huyo wa zamani.