Aliyekuwa rais wa LSK Nelson Havi sasa anasema kwamba maneno ya Rigadhi Gachagua yanafaa kuchukuliwa kwa uzito.
Havi kwenye mahojiano na runinga moja hapa nchini amesema kwamba Gachagua ndie aliyetoka ndani ya serikali na akikuambia kilicho ndani maneno yake usiyadharau.
"Huenda Rigathi Gachagua ni mamba anayetoka baharini na akikuambia huko chini ya bahari nyangumi ni mgonjwa usiyadharau maneno yake," alisema Nelson Havi.
Havi akizungumza ameeleza kwamba kama wao wana nia ya kusaidia serikali kutimiza malengo yao kwa serikali, ila Gachagua kuendelea kufunua mabaya ya serikali ni kazi nzuri na maneno yake yasipuuzwe maana yeye alikua mmoja wa hio serikali na huenda anjua mengi zaidi yetu.
Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua aliondolewa mamlakani baada ya hoja hio kupitishwa kwa mabunge yote mawili, bunge la kitaifa na bunge la seneti.
"Kuna baadhi ya mambo ambayo Gachagua anayazungumza labda bila uwangalifu na Hasira lakini haijalishi anachokisema. kuna uwezekano yana umuhimu.
"Yeye ni mtu maarufu kwa umati wa watu. anaweza kuwa na upungufu katika hukumu yake lakini huvutia umati wa watu. Jambo la kushangaza kuhusu Wakenya, wanamsikiliza yeyote anayewaigiza zaidi na Gachagua amebarikiwa na hilo,"
Rigathi Gachagua kwa upande wake ameapa kufanya lolote awezalo kuhakikisha kwamba Rais William Ruto ni rais wa muhula mmoja.
alipokua akizungumza kwenye mkutano wa ufunguzi wa makao mapya ya chama cha DAP-K chake Eugine Wamalwa, wakiwa wameandamana na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka alisema kwamba yeye ni mmoja wao na watafanya kazi kama timu moja'
"Sisi ni sehemu ya timu hii na tutatembea katika safari hii pamoja ili kuikomboa nchi hii. Tutatoa chochote kile na juhudi zozote muhimu kuhakikisha kuwa William Ruto ni rais wa muhula mmoja," alisema Gachagua.
Gachagua pia alimulaumu aliyekuwa bosi wake kwamba yeye ni dikteta na hakubali mashauri yeyote kutoka kwa mtu yeyote. Pia amesikika mara kwa mara akisema yeye ndiye aliyekua mtu wa pekee kusimama tofauti na mawaziri wengine. akidai kwamba ndilo lililofanya wakakosana na rais.