logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waziri Muturi: Rais Ruto lazima akomeshe utekaji nyara na mauwaji ya kiholela

Waziri wa utumishi wa umma Justine Muturi amerejea kwenye vyombo vya habari kwa mara ya pili kuzungumzia swala la utekaji nyara.

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri31 January 2025 - 13:52

Muhtasari


  • Rais ndie kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu na ana mamlaka ya kutosha.
  • waziri huyo amesisitiza kwamba hakuna sheria kwa taifa la Kenya ambao inaunga mkono swala la utekaji nyara na mauwaji ya kiholela kwa wananchi.


Waziri wa Leba Justine Muturi amekosoa serikali kuhusia na swala la utekaji nyara vijana. 

Waziri Muturi licha ya kuwa kwenye serikali alitofautiana na serikali alipozungumza na wanahabari akionesha kughadhabishwa na swala la kumuteka nyara mwanawe wa kiume wakati akiwa mwanasheria mkuu.

Mwezi Januari 12, muturi aliitaka wahusika kukoma kuwateka nyara vijana wa kenya.

Justine Muturi kwa mara nyingine amejitokeza huku akielekeza lawama moja kwa moja kwa rais William Ruto kwamba lazima akomeshe utekaji nyara kwa maana yeye ndie kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu na ana mamlaka ya kutosha.

waziri huyo amesisitiza kwamba hakuna sheria kwa taifa la Kenya ambao inaunga mkono swala la utekaji nyara na mauwaji ya kiholela kwa wananchi.

"Hili swala linafaa kuangaziwa kwa umakini sana, mzazi hawezi kaa akihuzunisha mtoto wake hayuko, ametekwa nyara, baada ya zaidi ya siku 40 anapatikana amekufa. kisha watu wanakaa mahali  wanapanga uchumi. wanapangia nani uchumi na watu wanauliwa.

Nilisema wakati mtoto wangu alitekwa nyara nilikua na bahati ya kumfikia rais, na akaamuru Nurdin Haji na akamuachilia, hawa akina mama ambao hawawezi kumfikia rais wafanye nini," alisisitiza waziri Muturi.

Spika huyo wa zamani ameeleza kwamba ana uhakika kwamba shughuli za utekaji nyara zinaendeshwa na maafisa wa usalama na wala si jambo la kujadili.

"Kwa hili swala rais ndie kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulizi, kwa hivyo bwana rais nataka sasa utangaze mwisho wa huu utekaji nyara na mauji, na pia ueleze kwa njia gani haya yalikua yakiendelea. unadhani hawa wazazi wanahisi vipi.

Watu hawawezi kuwa wanauliwa kila siku pasiposababu na tunajifanya tunajaribu kusuluhisha mambo ya DRC."  alisema Muturi huku akielekeza lawama kwa Rais Ruto.

Muturi amezungumza haya baada ya vijana waliotekwa nyara katika barabara ya mlolongo maarufu Mlolongo 3 kupatikana wakiwa wamefuka baada ya kukosekana kwa wiki kadhaa.

Baada ya maandamano ya Gen-z vinaja wengi walioendelea kuikosoa serikali hasa kwenye mitandao ya kijamii walitekwa nyara.

Wengine waliachiliwa baada ya siku kadha, wengine wakiwa bado hawajapatika mpaka sasa huku wengine wamepatikana wakiwa wameuliwa.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved