Raila Odinga afanyiwa maombi maalum kabla ya uchaguzi wa AUC
Ni maombi ambayo yaliandaliwa katika ukumbi wa Bomas yakiongozwa
na akina mama kusudio likiwa ni kumwombea Odinga. Bwana Odinga ambaye
aliandamana na mkewe bi Ida Odinga alionekana mpwamu na mwenye furaha wakati wa
hafla hiyo.
Kulingana na hotuba yake Raila Odinga alionyesha matumaini
makubwa ya kuchaguliwa akisema kuwa
alikuwa amefanya kampeni ya kutosha na kuzuru mataifa yote ya Afrika ambapo
alikutana na viongozi mbalimbali wa nchi tofauti waliomhakikishia kumpigia
kura.
Odinga aliwaonea wanawake Fahari huku akimshukuru mkewe kwa
kumjali pakubwa, Odinga alisema kuwa alikuwa na mkutano wa dharura ambao alisitahili
kushiriki lakini ukahairishwa akirejelea usemi kuwa mama Ida Odinga alimkumbusha
kuwa siku hiyo likuwa imetengwa kwa ajili yake .
Kulingana na mujibu wa maelezo ya Odinga alikuwa na Imani isiyotetereka
na hakikisho kuwa angeibuka mshindi alieleza historia fupi ya kulinganisha
mwaka wa huu wa 2025 na ule wa 2005 akisema kuwa uasisi na upatikaji wa Katiba mpya
na chama chake cha ODM ulifanyika katika
ukumbi huo wa Bomas hivo akawa anakumbuka siku hiyo kama siku ambayo itazaa
matunda .
Vilevile katika maelezo ya Odinga aliashiria pakubwa kuwa analifahamu
vyema bara la Afrika na matatizo yanayolikumba akisema kuwa matatizo yalio hapa
nchini Kenya ni sawa na matatizo ambayo yaliokuwa yakizikumba nchi nyingi za
afrika kama elimu,miundomsingi bora na mshikamano wa nchi za Afrika kwa jumla.
Raila alishauri akisema kuwa mapenzi yake ni kuona mataifa
yote yakifikia kilele cha ufanisi kwanzia nyumbani hadi sehemu nyingine za
ulimwengu aidha alionekana kumbariki gavana wa Nairobi bwana Johnson Sakaja
akimwita kijana wake usemi ambao ulifasiriwa kama njia ya kumbarki bwana Sakaja
na kumtakia kila la heri katika safari ya kutafuta ugavana kwa awamu ya pili iwapo
itawadia.
Zimesalia siku nne kabla ya uchaguzi huo kutimia ambapo iwapo Odinga atachaguliwa bila shaka masikani yake yatakuwa nchi ya Uhabeshi Addisababa kama taifa la Kenya tunasema kila la heri kwake Raila Mungu amkirimie baraka za ushindi.