Ruto akutana na mabalozi katika Ikulu ya Naiobi
Rais Wiilliam Ruto mapema leo Jumatatu alikutana na wawakilishi wa
mashirika mbalimbali ya nchi za kigeni wakiwemo mabalozi wa mataifa ya nchi za
kigeni katika Ikulu kuu ya Nairobi.
Ajenda ya mkutano huo ililenga kuzungumzia hali ya machafuko
nchini DRC ambako kumekuwa na hali ya utovu wa usalama katika taifa hilo.
Katika mkutano huo, rais Ruto alisistiza kuwepo kwa mazungumzo
ya upatanishi kama njia ya kipekee ya kuleta amani katika taifa la Kongo ambalo
ni mwanachama wa muungano wa jumuiya ya mataifa
ya afrika mashariki EAC na SADC.
Itakumbukwa vyema katika kikao kilichowaleta wanachama wote
wa SADC katika mkutano ambao ulifanyika Dodoma
Tanzania ambapo rais Amason Nangabo wa Zimbabwe
ambaye ndiye mwenyekiti wa SADC ili kuzungumzia hali tete ya usalama DRC.
Mkutano huo ulipofanyika rais William Ruto alisisitiza
kuwepo kwa umoja kati ya mataifa ya wanachama wote akikariri kuwa amani katika nchi
ya DRC haitaletwa kwa kutumia nguvu za jeshi bali kwa mazungumzo na mapatano ya
amani.
Taifa la DRC limekuwa likiisuta nchi ya Rwanda kwa madai ya kutuma
wanajeshi wake katika ukanda wa Kivu ulio kasikazini ya Kongo wakishirikiana na
kuundi la M23 ili kuuteka mji huo na kusababisha maafa na mahangaiko ya wananchi
jambo ambalo Rwanda kupitia kwa rais
Paul Kagame alipinga vikali.
Rais Ruto alipokuwa akihutubia umma uliojaa viongozi na
wawakilishi mbalimbali aligusisa pia suala la kuwa na hali nzuri ya mazingira
ya tabianchi akinadi kuwa utunzaji wa mazingira ni jambo la manufaa sana kwa
nchi yoyote ile.
Kiongozi wa nchi vilevile alizungumzia ushirikiano na umoja
wa mashirika ya nchi mbalimbali katika viwango mbalimbali akirejelea makubaliano
na mikataba mbalimbali ambayo inalenga kujenga ukuruba na wepesi wa kufanya
biashara bila vikwazo vyovyote.