Rais Ruto aungwa mkono na Marais wa Afrika kutaka
mabadiliko kwa mifumo ya kutoa mikopo
Rais Ruto aliungwaa mkono na marais wa afrika alipokuwa
akihutubia kongamano la Pamoja la 38 la marais wa Afrika mjini Addis Ababa
Ethiopia.
Rais Ruto katika hotuba yake alielezea kutoridhishwa kwake
na mifumo iliyopo ya taasisi za
kutathimini utoaji wa mikopo kwa Africa(AFCRA) alizungumza akirai kuwe na
mabadiliko katika mfumo huo ambao alisisitiza kuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko
bila shaka barala la Afrika litanufika ipasavyo na litajijenga sana.
Ruto alisema kuwa kuwa mfumo wa sasa umekuwa ukinyanyasa
baadhi ya mataifa ya afrika na kueneza ubaguzi kwa mataifa mengine jambo ambalo
alilitaja kama unyanyasaji kwa bara la Afrika ambao hautahiki kuwepo.
Rais Ruto ambaye ni mteetezi wa mabadiliko ya Umoja wa
Afrika alilalama kuwa licha ya Afrika kuwa na raslimali kubwa na nyingi
limezidi kuwa bara maskini licha ya utajiri mkuu linaomiliki na unaolikodolea macho ,alitaja kuwa Afrika ina
mashamba mengi tena yenye rotuba na
raslimali yenye fulusi nyingi.
Ruto alieleza kuwa taasisi za kutoa mikopo zimetoa tu mikopo
kwa mataifa mawil Afrikai tu licha ya mataifa mengi kuwa na uwezo wa kupokea na
kuchangia pakubwa.
Rais Ruto alisema kuwa kama bara la Afrika wanastahili na wanahitaji kuwe na mabadiliko iwapo
shughuli hiyo ya mabadiliko katika taasisi za kutoa mikopo na sheria
zitabadilika na kuwa na usawa wa haki bila shaka kama Afrika watakuwa katika mkondo
mwema.
Utafiti unaashria
kuwa bara la Afrika lina uwezo wa kujisimamia kiuchumi na kimaendeleo.
‘’Utafiti unaashiria kuwa kama bara la Afrika tukijitegemea
bila kuwa na mikopo Afrika inaweza zalisha dola bilioni 15.5 kiwango cha hela
ambazo zinaweza kufadhili miradi maalum ya serikali zote kwa asilimia 12,huku
asilimia 80 ikiangazia miundomsingi’’ Rais Ruto alieleza.
Viongozi wengine waliozungumza katika kongamano hilo la Pamoja
ni Abdelmadjid Tebbounce wa Algeria,Taye Selassie wa Ethiopia,Hakainde
Hichilema wa Zambia na naibu mwenyekiti wa AUC Monique Nsanzabaganwa.
Lengo kuu la kuanzisha mfumo imara kama Afrika ni kuzindua
taasisi ambayo ni ya kutathimini na kutoa mikopo kwa usawa bila ubaguzi,kuwa na
uwazi wa maendeleo katika bara la Afrika na hali halisi za mataifa ya afrika, Taasisi
ambayo itaangazia na kuzungumzia matatizo na matakwa ya Bara la Afrika.
Mfumo ambao ni imara kwa mataifa yote bali sio wa kutoa adhabu kwa mataifa bila kuangazia uhalisia wa mambo na vilevile taasisi ambayo inaangazia deta halisi na kutathimini uwezo wa mataifa mengi.