Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati ni mgonjwa mahututi.
Bosi huyo wa zamani wa IEBC amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi ambapo amekuwa akitibiwa kwa takriban wiki moja.
Chanzo kutoka hospitalini ziliambia Radio Jambo kwamba bosi wa zamani wa IEBC amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo.
"Tunafuatilia hali yake katika ICU," chanzo kilisema.
Ugonjwa ambao Chebukati anaugua unasalia kuwa faragha.
Chazo cha karibu cha familia kiliambia Radio Jambo kwamba bosi huyo wa zamani wa IEBC amekuwa akitibiwa nyumbani na alipelekwa katika Hospitali ya Nairobi baada ya hali kuwa mbaya.
Chebukati alihudumu kama mwenyekiti wa IEBC kwa muhula mzima wa miaka sita na alistaafu Januari 2023.
Aliongoza Uchaguzi Mkuu wa 2017 na 2022