Viongozi wa bara la Afrika katika ukumbi wa Nelson Mandela Ethiopia.
Baada ya kipindi cha uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa AUC
kutamatika, baadhi ya wachanganuzi wa masuala ya diplomasia na kisiasa wametoa sababu za Kenya kupoteza
katika uchaguzi huo.
Wachanganuzi mbalimbali wamejitokeza na kuweka bayana baadhi
ya masuala ambayo huenda kama taifa hayakutiliwa maanani na kusababisha mwaniaji wa
Kenya kufeli.
Seneta Richard Onyonka ambaye pia ni mtaalamu katika masuala
ya kidiplomasia alipohojiwa na kituo kimoja cha Habari nchini ili aeleze kwa
maoni yake chanzo kilichosababisha Kenya kupoteza katika uchaguzi wa AUC.
Bwana Onyonka alifafanua kuwa sababu ya kwanza ambayo
ilichangia Kenya kupoteza katika kinyang’anyiro hicho ni kuwa na sera potovu za
kidiplomasia kuhusu siasa zetu za kikanda na masilahi ya mataifa mbalimbali duniani.
Vilevile alifafanua wazi kwa kusema kuwa Vita katika taifa
la Jamhuri ya Kongo pia vilichangia pakubwa ambapo rais William Ruto ndiye
mwenyekiti wa ukanda wa Afrika Mashariki (EAC),alipoitisha mkutano wa Pamoja kushughulikia
suala hilo ilishangaza rais wa Kongo hakuhudhuria
mkutano huo.
Kutokana na rais wa Kongo bwana Felex Tsisekedi kususia mkutano wa ukanda wa Afrika
Mashariki na kuhudhuria ule wa SADK ilikuwa ni ishara kuwa mambo hayakuwa
yanaendelea vyema kutokana na suala la
kuleta amani katika taifa lake la Kongo.
Inasemekana kuwa pia katika matamshi ya rais William Ruto
miezi kadhaa iliyopita kuhusu vita vya Israeli na Palestine alinukuliwa waziwazi rais Ruto akipongeza taifa la Israeli
na kuahisi Palestine usemi ambao haukuchukuliwa vyema na viongozi ambao
wanaegemea dini ya kiislamu.
Jambo ambalo lilichochea mataifa yanayoegemea dini ya
kiislamu kuchukua mkondo tofauti na kumpigia kura mwaniaji wa Djibout Mohamoud
Ali Youssouf ambaye alikuwa mwisilamu,kutokana na kigezo hiki viongozi wengi wa
mataifa mbalimbali waliamua kuchukua misimamo yao tofauti.
Wakili
PLO Lumumba katika maoni yake
alieleza kuwa kuanguka kwa Raila katika
kiti cha uenyekiti wa AUC si wa binafsi bali ni wa Taifa kwa jumla, kwani hiyo
iliashiria tabia na sura ya taifa katika nchi za nje.
Vilevile alieleza kuwa ni kutokana na kufeli kwa kitengo cha
masuala ya diplomasia kutofanya urafiki wa karibu uhusiano mwema na mataifa
mengine ya nje akisema kuwa huo sasa ndio mwamko mpya wa kujenga uhusiano mwema
na mataifa ya nje na kuteua watu bora zaidi.