Serikali ya Sudani iliikosoa vikali serikali ya Kenya kutokana
na hatua yake ya kulikaribisha kuundi la waasi wa RSF kutia Saini ya
makubaliano na washirika wao jijini Nairobi.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje
ya Sudani ilisema kuwa hio ni uvunjaji wa wajibu wa Taifa la Kenya chini ya sheria za
kimataifa,mkataba wa umoja wa mataifa ,misingi ya umoja wa Afrika na mkataba wa
kuzuia uhalifu wa kimbari.
Sudani ilidai kuwa Kenya ilikiuka ahadi yake ya kuzuia shughuli za uadui dhidi ya Sudani kutoka katika ardhi yake.
‘’Hatua hiyo ya serikali inapinga kanuni za ujirani mwema
vilevile inakwenda Kinyume na ahadi zilizotolewa na Kenya katika ngazi ya juu ya
kutoruhusu shughuli zozote kufanyika katika ngome yake taarifa hiyo ilieleza’’.
Serikali ya Sudani ilipuzilia mbali madai ya kuwa shughuli
za RSF jijini Nairiobi hazikuwa na mashiko yoyote na kutaka jamii ya kimataifa
kulaani kitendo hicho.
Wanamgambo wa RSF wamekuwa na mzozo na serikali tawala ya Sudani na mara kwa wamekuwa wakitishia kuuunda serikali mbadala
ndani ya Sudan wakisema kuwa shughuli hiyo ingefanyikia jijini Nairobi.
Makubaliano ambayo RSF
na makundi husika yalikusudia yawe
na maafikiano ya utendakazi wa kudumu ikizingatiwa kuwa makundi ya washirika
wake ambayo yana silaha yalilenga kuunda
serikali mbadala ya Amani na Umoja katika maeneo ambayo RSF inadhibiti.
Walitoa madai kuwa makubaliano na washirika wao wa karibu
yalilenga utoaji wa huduma za afya,ulinzi,na kuwa na uhalali wa kuendesha
shughuli zao bila matata.
Hata hivyo washikadau ambao wanahusika na mchakato huo wa
utekelezaji wa mkataba huo hawakueleza makubalianao hayo yalikusudia nini ila
kamati husika iliwahi sema kuwa lengo lao lilikuwa ni kurejesha serikali halali
ambayo ilipinduliwa na wanamgambo wa kiislamu.
Kulingana na wao walisema hiyo ilikuwa njia moja wapo ya kujumuisha
kila mmoja katika serikali ambayo itakuwa ya umoja na amani kwa uwendelevu
hivyo wengi wanaliangazia suala hilo kwa ukaribu kutaka kujua ni nini
kitachofuata.