
Kulingana na ujumbe kutoka kwa afisi ya Mkuu wa Waziri Musalia Mudavadi msuada wa upokezaji wa mamlaka unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni unalenga kulinda demokrasia ya siku za usoni.
Msuada huo uliidhinishwa na baraza la mawaziri mnamo Desemba 17,2024 na utalainisha mchakato wa upokezanaji wa mamlaka kutoka kwa utawala mmoja hadi mwingine bila matata.
Msuada huo unalenga kuweka sheria ya wazi na mchakato imara
ambao utasaidia katika shughuli ya kupokezana mamlaka.
Lengo kuu la msuada huo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na
uwazi na usawa wa kuchukua na kupokezana mamlaka ya urais Pamoja na sherehe
ambazo zinaambatana na kuchukua hatamu za
uongozi kulingana na kifungu cha Katiba nambari 141 cha upokezenaji wa mamlaka
au uongozi kabla na baada ya uchaguzi.
Msuada huo uliasisiwa na idara ya masilahi ya bunge katika ofisi ya mkuu wa mawaziri.
Msuada huo ulifafanua ukisema kuwa rais aliyoko Madarakani
atapokeza mamlaka kwa rais mteule chini ya kifungu nambari
141 ama 146 cha Katiba ya Kenya.
Naibu wa rais mteule atachukua mamlaka ya afisi chini ya
kifungu cha Katiba nambari 148, mwanasheria mkuu wa serikali atachukua hatamu za
uongozi kwa kulingana na kifungu cha Katiba
nambari 156 ,huku mawaziri wakila viapo vya ofisi chini ya kifungu nambari 152, huku makatibu wa kudumu katika kifungu nambari 155 huku katibu wa baraza la mawaziri akipokea kiapo chini ya kifungu 154
Mchakato wa kubadilishana hatamu za uongozi utaanza siku tisini kabla ya kura ya rais
ipigwe na imalizike siku tisini baada ya
rais mteule kuchukua hatamu za uongozi ama baada ya kamati andalizi kupeleka
ripoti yake katika bunge la taifa yoyote ile itakayo tangulia.
Kamati andalizi ya mchakato huo ambayo husimamia serikali
ya mpito hujumuisha watu wafuatao mkuu wa utumishi wa Umma ambaye ndiye mwenyekiti
wa kamati, wanasheria mkuu wa serikali, katibu wa baraza la mawaziri, makatibu katika idara za usajili wa watu, usalama wa ndani, ulinzi, masuala ya kigeni,fedha,Habari na mawasiliano
na utamaduni.
Wengine watakuwa mkuu wa majeshi,mkurugenzi mkuu wa
kitengo cha ujasusi, insipekta mkuu wa polisi, karani wa bunge la kitaifa na
seneti, msajili mkuu wa mahakama na wajumbe wengine tisa watakaochaguliwa na
rais mteule.