logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbunge George Koimburi Atoroka Kwa Pikipiki Kwa Hofu Ya Kutekwa Nyara

Alipokuwa akielekea kwenye gari lake na mawakili wake, kundi la wanaume waliovalia kiraia walidaiwa kujaribu kumshika mkono

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri20 February 2025 - 14:49

Muhtasari


  • Koimburi, anaripotiwa kutoroka kwa pikipiki ili kuepuka kile ambacho wakili wake, Ndegwa Njiru, ameelezea kama jaribio la "utekaji nyara."
  • Akihisi hatari, Koimburi na timu yake walikimbilia upande mwingine, ambapo anaripotiwa kupanda pikipiki na kuondoka haraka eneo hilo.

Mbunge George Koimburi baada ya kikao cha mahakama

Mbunge wa Juja, George Koimburi, anaripotiwa kutoroka kwa pikipiki ili kuepuka kile ambacho wakili wake, Ndegwa Njiru, ameelezea kama jaribio la "utekaji nyara."

Kwa mujibu wa Wakili Njiru, mbunge huyo aliponea chupuchupu kutekwa nyara nje ya Mahakama ya Kiambu.

Koimburi, ambaye aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu ya Sh200, 000 Jumatano, alifika mahakamani Alhamisi kwa maelekezo kuhusu iwapo atakubali kusomewa mashtaka ya kukosa kuhudhuria vikao vya awali vya mahakama.

Baada ya kikao cha mahakama, mbunge huyo alizungumza na wanahabari akiwa na wakili wake, Seneta wa Makueni Dan Maanzo, na washirika wengine.

Hata hivyo, wakati wa mkutano huo, alionekana akizungumza na afisa mmoja, jambo lililomfanya kusitisha mkutano ghafla.

Alipokuwa akielekea kwenye gari lake na mawakili wake, kundi la wanaume waliovalia kiraia walidaiwa kujaribu kumshika mkono, lakini walizuiliwa haraka na mawakili wake.

Akihisi hatari, Koimburi na timu yake walikimbilia upande mwingine, ambapo anaripotiwa kupanda pikipiki na kuondoka haraka eneo hilo.

Mapema mahakamani, hakimu aliratibu tarehe 25 Februari kama siku ya kutolewa kwa uamuzi kuhusu iwapo masharti yake ya dhamana yatabadilishwa.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved