logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wafisadi, wezi na waongo wamelaaniwa, Mchungaji Lai asema

Willifred Lai mchungaji wa kanisa la Jesus Celebration Centre liliko Bamburi Mombasa alihubiri kuhusu ufisadi,wizi na kiburi .

image
na Evans Omoto

Yanayojiri24 February 2025 - 10:48

Muhtasari


  • Katika Mahubiri yaliohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu akiwemo rais Ruto, Lai aliweza kuwahubiria waumini kwa kuwaeleza maovu ambayo hutendwa na binadamu duniani.
  • Wakati ambapo mchungaji alikuwa anahubiria waumini waliokuwa kanisani walionekana kuchangamkia kauli na mahubiri .

Wilfred Lai

Mchungaji Lai ahubiri kuhusu maadili

Willifred  Lai mchungaji wa kanisa la Jesus Celebration Centre liliko Bamburi Mombasa alihubiri kuhusu ufisadi,wizi naa kiburi miongoni mwa Viongozi.

Katika Mahubiri yaliohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini akiwemo Rais Ruto, mchungaji Lai aliweza kuwahubiria waumini kwa kuwaeleza maovu ambayo hutendwa na binadamu duniani.

Mchungaji aliweza kuhubiri kwa mafumbo huku akiashiria kuwalenga watawala ambao hutumia nafasi na hadhi zao kuwadhulumu wanyonge kwa kutangaza sera za uongo na kutowajibika ipasavyo.

Mchungaji Lai kulingana na mujibu wa mahubiri yake aliweza kusema kuwa viongozi wale ambao wanaeleza sera za uongo na kula mali ya umma hawatafanikisha malengo yao bali watafariki kabla ya kutimiza kile ambacho walikidai kama kuendeleza ajenda za uongo na ufisadi.

Mchungaji Lai alisema Viongozi ambao wanadhani kuwa kukuwa tajiri ni lazima uwe fisadi na uwaibie raia au wananchi alisema kuwa kwa kufanya hivyo walikuwa tayari wamelaaniwa na kumuibia Mungu kwani ufalme wa Mungu si wa wanyang’anyi.

Wakati ambapo mchungaji alikuwa anahubiria waumini waliokuwa kanisani walionekana kuchangamkia kauli na mahubiri ya mchungaji wakisema kuwa yalikuwa ni mahubiri na injili kali na takatifu amabayo ilikusudia kuwanyoosha wale ambao walikuwa na mienendo potovu wabadilike.

Injili iliweza kujikita katika masuala ya ufisadi, kiburi, majigambo na maringo mchungaji akishauri wakristo kubadilisha mienendo yao hasi ambayo haimufurahishi Mungu, mchungaji alionekana kuwalenga wakiristo mbalimbali ambao wamekuwa wacha Mungu ila mara nyingi wamekuwa na tabia kama za Lumbwi.

Injili ya aina hii ilikuwa ikiendelezwa na watumishi wa Mungu kila mahali wanapokutana ili kuwawosia  viongozi kujali na kuhudumia wananchi kwa kutimiza ahadi walizo ahidi wananchi.

Itakumbukwa kuwa askofu bwana Antony Muheria kwa wakati mmoja alinukuliwa akitoa matamshi ya kuishauri serikali iweze kutekeleza wajibu wake kwa kumhudumia mwananchi kwa uzalendo wa hali ya juu.

Wosia wa bwana Muheria ulipokelewa  kimseto na baadhi ya viogozi serikalini waliomkashifu kwa kuasi mambo ya dini na kuingilia siasa za taifa wakimtaka ajiuzulu na ajitose siasani bila kuogopa


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved