logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkenya Akamatwa Marekani kwa Kumuua Mkewe kwa Risasi

Wakati wa mauaji hayo, watoto wawili wa wanandoa hao walikuwepo ndani ya nyumba.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri25 February 2025 - 15:43

Muhtasari


  • Gitau mwenye umri wa miaka 42, alikamatwa katika kambi ya kijeshi ya Fort Cavazos baada ya msako wa polisi.
  • Polisi wanaamini kuwa tukio hilo lilichochewa na mzozo wa unyanyasaji wa kinyumbani.

Mshukiwa John Gitau Mwangi

Polisi katika jimbo la Texas, Marekani, wamemkamata Mkenya anayeshukiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi mara kadhaa nyumbani kwao.

John Gitau Mwangi, mwenye umri wa miaka 42, alikamatwa katika kambi ya kijeshi ya Fort Cavazos baada ya msako wa polisi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Polisi ya Killeen, mwathiriwa alikuwa mwanamke Mkenya mwenye umri wa miaka 37.

Polisi walipokea taarifa mnamo Ijumaa, Februari 21, 2025, mwendo wa saa moja na dakika 16 usiku, wakiombwa kufanya ukaguzi wa maendeleo katika makazi ya familia hiyo kwenye mtaa wa Lakecrest Drive.

Walipofika, walimpata mwathiriwa akiwa na majeraha mabaya ya risasi.

Licha ya juhudi za wahudumu wa afya kuokoa maisha yake, mwanamke huyo alithibitishwa kufariki saa tatu na dakika 29 usiku na Hakimu Nicola James. Majina yake hayajatolewa hadharani huku familia yake ikisubiriwa kufahamishwa.

Polisi wanaamini kuwa tukio hilo lilichochewa na mzozo wa unyanyasaji wa kinyumbani.

Wakati wa mauaji hayo, watoto wawili wa wanandoa hao walikuwepo ndani ya nyumba lakini hawakutendewa madhara.

Ripoti zinaonyesha kuwa watoto hao huenda hawakuelewa kilichotokea.

Baada ya tukio hilo, mshukiwa alitoroka kutoka eneo la uhalifu lakini baadaye alikamatwa na maafisa wa upelelezi wa Robbery-Homicide Unit waliokuwa wakimsaka.

Kwa sasa, anazuiliwa katika Gereza la Killeen City akisubiri mashitaka rasmi, ambapo anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha jela au hata adhabu ya kifo chini ya sheria za Texas.

Haya yanajiri takriban miezi mitano baada ya mwanamume mwingine Mkenya aliyeshukiwa kumuua mpenzi wake nchini Marekani mwaka wa 2023 kurejeshwa Massachusetts, Marekani ambako alikabiliwa na shtaka la mauaji ya daraja la kwanza.

Kelvin Kang’ethe alisafirishwa kutoka Kenya hadi Marekani mnamo Septemba 2, 2024 baada ya kukamatwa Nairobi.

Bw Kang’ethe, 40, alidaiwa kumuua mpenzi wake Margaret Mbitu kati ya Oktoba 30 na Novemba 1, 2023. Marehemu alikuwa msaidizi wa afya ya nyumbani katika mji wa Halifax, Massachusetts.

Mshukiwa kisha alikimbilia Kenya na hati ya kukamatwa kwake ikatolewa na mahakama ya Wilaya ya Chelsea, Massachusetts, ambayo ilifuatiwa na ombi la kurejeshwa kwa Bw Ingonga.

Kang’ethe alikamatwa mnamo Januari 30, 2024, Parklands, Kaunti ya Nairobi, lakini alitoroka kutoka kizuizini kabla ya kukamatwa tena.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved