Gavana wa kaunti ya Naironi Arthar Johnson Sakaja amejitokeza ili kufafanua zaidi mvutano ulioko baina ya serikali ya kaunti ya Nairobi na kampuni ya umeme ya Kenya Power.
Vuta, nikuvute kati ya idara hizi mbili za serikali imekuwepo kwa muda sasa huku kila upande ukivuta kwao ili kuonesha ubabe, huku idara zote zikisisitiza kuhusu kudaina mabilioni ya pesa.
Kampuni ya KPLC inailaumu serikali ya kaunti kwa kuwakatia maji pamoja na kumwaga taka mbele ya ofisi yao huku serikali ya kaunti ikilaumu "Kenya Power" kwa kuwakatia umeme.
Sakaja kwa upande wake akizungumza na kituo cha Radio Jambo Jumatano asubuhi alileza kwamba suala hilo halifai kuwa hivyo ila kutokana na madharau ambayo wamepata kutoka kwa hio kampuni, hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kufanya walivyofanya.
Kulingana naye, maagizo ya kumwaga taka hayakuwepo.
"Ni kitu ambacho si kizuri, haifai kuwa hivyo kati ya idara mbili za serikali ambazo zinahudumia wananchi. Ijumaa tulikata maji na siweji katika ofisi zao na tukatuma magari 'manne' kukinga ofisi zao. Mambo ya kumwaga taka niliwakemea sana. Takataka haikuwa inafaa imwagwe, ukiona Sakaja amefika hapo amefika mwisho, tumezungumza, tumeandika barua hawaoni," alifafanua Sakaja.
Gavana huyo wa Nairobi alieleza kwamba wanadai kampuni hio ya umeme zaidi ya bilioni nne huku akipuuzilia mbali madai ya KPLC ambayo walifichuwa kwamba wanadai zaidi ya bilioni tatu kutoka kwa serikali ya kaunti baada ya kudinda kulipia gharama ya umeme tangu mwaka 2022.
"Jambo la kukera ni kwamba tunadaiana, tunawadai milioni 4.8 ambayo hawajawahi kulipa wala kuwa na mpango wa kulipa. Wanafaa kutulipa koti iliamua hivyo. Ile ambayo wanatudai ni milioni 1.5. Walikuwa wanasema 3 milioni. nikasema ... tufanye verification. Hao ndugu zetu wakikuambia deni yako ni hii upinge, wanasema lipa kwanza," alifafanua zaidi.
"Tulikuwa na mkataba tukakubalia kwamba tutalipa 1.5, na tukaana kulipa kila mwezi milioni 50, na wakati mwingine milion100... kwa wiki moja tulikosa stima...," Sakaja aliendelea.
Gavana pia ameeleza kwamba tayari wako mbioni kutafuta suluhisho huku akifichua kwamba wamepanga mkutano utakaowaleta pamoja ili kujaribu kutatua suala hilo. Wakati huo pia ameweka wazi kwamba tayari wameyaondoa magari ila jambo ila maji litahitaji makubaliano mazuri.
"Asubuhi hii tuna mkutano pamoja mkubwa wa utumishi wa uma, watu wa Kenya Power na mimi pia nitakuwa kwa huo mkutano na watu wangu.ili tutafute suluhisho.... Magari tumetoa leo lakini mambo ya maji na siweji lazima waanze kulipa kwanza,' alisema gavana huyo wa muungano wa Kenya Kwanza.