KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Februari 26, 2025.
Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na mbili jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kakamega, Kisii, Embu, Meru, Kiambu, Kitui, Kilifi, na Kwale.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kangemi na UMOJA 2 zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na mbili jioni.
Soko la Lukume katika kaunti ya Kakamega litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Rianyoka na Nyamasibi katika kaunti ya Kisii yataathirika kati ya saa mbili unusu na saa kumi alasiri.
Eneo la Ishiara Polytechnic katika kaunti ya Embu litaathirika kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Meru, sehemu za maeneo ya Ntugi, Kisima, na Marania zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Ndenderu Road, St. Linda, Gatong'ora, na Ruaka katika kaunti ya Kiambu pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Soko ya Thitani na eneo la Kanya katika kaunti ya Kitui pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Mwango, Mtondia, na Tezo katika kaunti ya Kilifi pia yataathirika kati yya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Hospitali ya Msambweni katika kaunti ya Kwale pia itaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.