KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 27, 2025.
Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Machakos, Murang'a, Nyeri, Embu, Kirinyaga, Kakamega, Migori, na Narok.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kasarani, Westlands, Jogoo Road, Mombasa Road, na Kilimani zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jjoni.
Maeneo ya soko la Mukinduri na Kiamwaki katika kaunti ya Kirinyaga yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Suswa na Duka Moja katika kaunti ya Narok yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.
Soko la Makunga na lile la Lutaso katika kaunti ya Kakamega yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Machakos, sehemu za Kangundo Road zitakosa umeme kati ya saa tatu na saa nane alasiri.
Maeneo ya Kamahuha na Makuyu katika kaunti ya Murang'a yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Charity na Embaringo katika kaunti ya Nyeri zitaathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Frevane Hospital na Nthokis katika kaunti ya Embu pia yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na kumi na moja unusu alasiri.
Maeneo ya Kehancha, Ntimaru, na Taranganya katika kaunti ya Migori yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi alasiri.