Tukio hilo lililotokea mnamo Februari 25,2025 la Kaunti ya
Nairobi Kwenda kumwaga taka mbele ya lango la Kampuni ya KPLC limekashifiwa na
wengi.
Kama kile ambacho serikali ya Kaunti ya Nairobi ilisema
kupitia kwa kiongozi wa Kaunti bwana Sakaja ni kuwa jambo hilo lilitokea kwa sababu
ya kuwepo kwa mzozo wa madeni kati ya pande
zote mbili husiika.
Gavana Sakaja akieleza hasa chanzo kilichosababisha matukio
hayo kujiri alisema kuwa tukio hilo lilitokea kwa sababu ya kutowajibika kwa
Kampuni ya KPLC na kuonyesha ari ya kulipa deni walilokuwa wakidaI Kampuni hiyo
jumla ya shilingi bilioni 4.8.
Kwa Upande mwingine Kampuni ya Kenya power ilikuwa ikidai
serikali ya kaunti ya Nairobi shilingi bilioni 1.5 kwa hivyo ilipaswa kuwe na
maelewano kabla ya hatua zozote kuchukuliwa.
Hata hivyo kulingana na usemi wa Gavana mwenyewe alikiri akisema
kuwa Kama kaunti sheria inawapa mamlaka ya kutoa notisi ya kudai hela au deni
kwa kumwarifu unayemdai kwa muda wa siku tisini(90) kabla ya hatua yoyote
kuchuliwa.
Hata hivyo iwapo siku tisini zitakamilika pasi jambo lolote
kutokea serikali itachukua jukumu la kukata maji na kusitisha shughuli za usafi
wa mabomba ya mitaro katika Kampuni husika Gavana alidadavua vizuri.
Hata hivyo tukio la kumwaga taka katika lango la Kampuni ya
KPLC kwa ishara ya kuonyesha ghadhabu halikufaa tena ni kinyume cha sheria za
kaunti na ni tukio la aibu kwa kaunti na kwa Kiongozi wa jiji.
Kutokana na hilo suala viongozi mbalimbali waliweza kutoa
hisia zao mseto kuhusu tukio hilo la umwagaji taka katika lango la KPLC.
Mbunge wa mbeere kasikazini Geoffrey Ruku alilaani kitendo
hicho cha umwagaji wa taka akikisawiri kama kitendo cha uhayawani na kutaka
hatua kali zichukiliwe dhidi ya Gavana kwa kuvunja sheria kwa kuwasilishwa
kortini.
Rosa Buyu mbunge wa Kisumu magharibi kwa upande wake alitoa wito wa Gavana kuwadhibikia matukio yake kwa kuwaadhibu wananchi wa Nairobi wasio na hatia yoyote kwa kile alikisawiri kama kuonyesha hasira zake kwa Kampuni ya KPLC kwa njia mbovu.
Willis Otieno naibu kiongozi wa chama cha Safina naye
alisema kuwa Gavana alistahiki kufikishwa mahakamani kwa makosa ya uchafuzi wa
mazingira na kutatiza hali ya maisha na ya wafafanyakazi husika.
Ni mzozo ambao ulitokea ila duru za kuaminika ziliarifu kuwa
kulikuwa na mkutano wa mapatano ili kutatua na kupata mwafaka wa mgogoro huo.