Marekani yasema iko huru kuchunguza ushirikiano wa raslimali muhimu ya madini na
serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).
Huku Kongo ikitaka usaidizi wa Marekani katika vita vyake vinavyoendelea dhidi ya waasi
wanaodhibiti asilimia 10% ya eneo la Jamhuri ya Kidemokrrasia ya Kongo kulingana
na mujibu wa ripoti kutoka Kinshasha.
Hatua hio inafuatia Kinshasa kutangaza Mipango ya kuimarisha
jeshi katika suala la fedha na silaha na kuiwezesha kutekeleza hilo.
DRC ambayo ina utajiri
mkubwa wa madini ya Kobalti,Lithiamu na Uraniam miongoni mwa madini
mengine imekuwa ikipambana na waasi wa M23 wanaungwa mkono na na nchi ya Rwanda
ambayo imeteka maeneo mengi mwaka huu.
Katika ushirikiano huu serikali ya Kinshasa inapania kuzipa kampuni
za Marekani haki ya kuchimba na kusindika madini ya thamani na kulipia msaada
huo. Serikali ya Kinshasha ilihitaji
msaada wa kijeshi,mafunzo Pamoja na
vifaa vya kijeshi.
Mwishoni mwa mwezi uliopita serikali ya Kinshasa iliiomba
Marekani kuwekeza katika nchi yenye hifadhi ya madini ya thamani ya dola trilioni 24 ambazo hazijatumiwa .
Madini ni muhimu kijeshi,Kiteknologia na nishati kulingana na barua ya serikali ya Kinshasa
kwa serikali ya Marekani.
‘’ Kuna nia ya sisi kubadilisha washirika wetu’’ msemaji wa
serikali ya DRC Patrick Muyaya alisema juma lililopita.
‘’Ikiwa leo wawekezaji wa Marekani wana nia ya kuja DRC ni wazi watapata nafasi DRC ina akiba ambayo
inapatikana na itakuwa vizuri kama mitaji ya Marejkani inaweza kuekeza hapa ‘’alisema.
Barua ya DRC inaomba kwamba Rais Trump wa Marekani binafsi awepo kwenye mijadala kuhusu ushirikiano huu na
kuamba mkutano kati ya Rais Trump na rais Tshisekedi utakuwa muhimu katika kufanikisha ushirikiano
huo.
Akielezea kuhusu ushirikiano wa Marekani na DRC Tina Salama
msemaji wa Rais Tshisekedi aliandika kwenye ukurasa wa X kwamba Tshisekedi
alialika Marekani yenye kampuni zinazonunua vifaa vya msingi kutoka Rwanda vinavyoporwa nchini DRC na kuingizwa nchini Rwanda ambapo kwa sasa
wanaiomba Marekani inunue kutoka kwa mmiliki halisi wa madini.
Kwa upande mwingine Rwanda ilisema kuwa madini ya DRC si
sababu ya mzozo wake na DRC na kwamba
wanaochimba na kufaidika nayo ni
Kampuni kutoka magharibi. Rwanda pia ilikanusha
kusaidia kundi la waasi wa m23.