Safari ya Rais Ruto ya kuzindua miradi ya maendeleo katika sehemu mbalimbali za viungaji vya jiji kuu la Nairobi imekuwa na changamoto tele kwa wakazi wa maeneo lengwa.
Kulingana na matukio yaliopita katika msafara wa Rais William Ruto wa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya taifa katika sehemu za Mathare,Ruaraka,Kamukunji na Sehemu za mto wa Nairobi ulikumbwa na matukio mengi ya anasa.
Mnamo Jumatatu Rais aliongoza kampeni za kusafisha Mto Nairobi ili kuwe na mazingira safi na mtiririko wa maji taka ulio mwema na ambao utarahihisha maisha mepesi kwa wakazi wa Nairobi vilevile katika ziara hiyo rais aliweza kuvumisha mradi wa Nyumba za bei nafuu kwa wananchi.
Hayo yote yalipokuwa yakiendelea kulitokea changamoto kadhaa ambazo ziliwatatiza wananchi wengi ambao walikabiliwa na hasara iliyosababishwa na ziara hizo za Rais.
Mwanzo kabisa sehemu zile ambazo rais alikuwa akizuru wafanyabiashara wa upande huo wamekuwa wakifunga biashara zao kwa kuhofia kuibiwa na wahuni au watu wasiowajua ambao huwa katika misafara ya Rais Ruto.
Isitoshe mara nyingi Rais anapokuwa katika hafla kama hiyo ya uzinduzi wa miradi mbalimbali Barabara nyingi huwa zinafungwa hivyo kulemaza shughuli za usafiri na kusababisha msongamano wa Magari kila katika kipindi hicho.
Katika visa vya hivi punde ambayo viliweza kuwaatua nyoyo watu wengi ni visa vya kinyama ambavyo vilishuhuidiwa katika hafla ya safari ya Rais katika sehemu za Kamukunji,Mathare,Barabara kuu ya Thika, Barabara ya Outering na katika Barabara ya Juja.
Katika sehemu hizo nilizotajwa kulishuhudiwa uvamizi wa kimabavu kutoka kwa vijana wa kihuni waliochukua nafasi ya ziara ya Rais ya Maendeleo kupora,kuiba na kunyang’anya wananchi hadharani na hata wengine kupigwa kitutu na kuumizwa.
Vijana na watu walionaswa katika Video za kamera walionekana wakipenyeza katika magari ya watu yaliokuwa yameegezwa katika Barabara yakisubiri kuondoka,vijana hao ambao wana ujasiri kama simba walionekana wakichopoa simu kutoka kwa magari vilevile kwa wapitanjia kwa njiia ya unyang’anyi wa lazima.
Matukio hayo yalipokua yakitekelezwa juhudi za maafisa wa
polisi kuwadhibiti ziliambulia patupu kwani vijana hao walikuwa ni genge la wahalifu
ambao kulidhibiti ilikuwa ni nadra kwa wakati huo ikizingatiwa kuwa maafisa wa
usalama walikuwa na kibarua cha kuhakikisha kuwa mikakati na mipango ya Rais inaendeshwa
jinsi ilivyoratibu chini ya usalama wao.