logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu kwa kina kuhusu hukumu ya kunyongwa katika Mataifa ya Afrika Mashariki

Kwa Afrika, adhabu ya kifo haitekelezwi sana, licha ya hukumu ya adhabu hiyo kutolewa katika mataifa mengi

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri17 March 2025 - 16:19

Muhtasari


  • Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linakiri kuongezeka kwa visa vya watu kunyongwa.
  • Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kuna visa 1,153 vya adhabu ya kunyongwa mwaka 2023 kwa ujumla.

Death Penalty
Kwa Afrika, adhabu ya kifo haitekelezwi sana, licha ya hukumu ya adhabu hiyo kutolewa katika mataifa mengi kwenye bara la Africa.

Nchini Kenya, hukumu ya kifo ilitekelezwa kwa mara ya mwisho mwaka 1987 kufuatia jaribio la kuipindua serikali la 1982, ambapo Hezekiah Ochuka alinyongwa kwa kosa la uhaini.

Mwaka 2021, watu 601 walikuwa wamehukumiwa kifo na hukumu nyengine 14 za kifo zilitolewa mwaka huohuo. Hukumu nyingi hazikuwa za dawa za kulevya.

Tanzania, inatajwa kutotekeleza adhabu hiyo kwa miaka karibu 30, ingawa idadi ya walihukumiwa kunyongwa kwa makosa mbalimbali, ikivuka 600, kwa mwaka 2023.

Ingawa kosa la mauaji, linabeba idadi kubwa ya wanaohukumiwa kunyongwa Tanzania kuliko kukutwa na dawa za kulevya.

Nchini Uganda, Bunge la nchi hiyo lilipitisha sheria inayopinga hukumu ya adhabu ya kifo kwa baadhi ya uhalifu. Wakati huo kulikuwa na wafungwa wapatao 133 ambao walihukumiwa kunyongwa lakini ikipita zaidi ya miaka 20 bila kunyongwa ama kutekelezwa kwa adhabu hiyo.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International inakiri kuongezeka kwa visa vya watu kunyongwa katika utekelezaji wa adhabu ya kifo duniani kote.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kuna visa 1,153 vya adhabu ya kunyongwa mwaka 2023 kwa ujumla, ongezeko la asilimia 31 kutoka 883 mwaka 2022. Ni idadi ya juu zaidi kunakiliwa na Amnesty International tangu 2015, wakati watu 1,634 walinyongwa. Hivi ni visa vya kunyongwa kwa ujumla.

Adhabu ya kifo haitumiki kabisa katika nchi 112, ikilinganishwa na 48 mwaka 1991. Nchi sita zilikomesha hukumu ya kifo kikamilifu, au kwa sehemu, mnamo 2022. Nne - Kazakhstan, Papua New Guinea, Sierra Leone na Jamhuri ya Afrika ya Kati - ziliifuta kabisa. Guinea ya Ikweta na Zambia zilisema itatumika tu kwa uhalifu mkubwa zaidi.

Mnamo Aprili 2023, bunge la Malaysia pia lilipiga kura ya kuondoa hukumu ya kifo ya lazima kwa makosa 11 makubwa ya uhalifu , yakiwemo mauaji na ugaidi. Bunge la Ghana lilipiga kura ya kukomesha kabisa hukumu ya kifo mnamo Julai 2023.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved