Matukio ya amri ya Kunyongwa kwa Mkenya Margaret Nduta Macharia
aliye na umri wa Miaka 37 kule Vietinamu ilibuua hisia na uangalifu mkali
kuhusu sheria za nchi za Ulaya kuhusu ulanguzi wa Dawa za Kulevya.
Nduta alishikwa mnamo
Machi, 6 2025 baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo mbili za
mihadarati aina ya Kokeini kutumia uwanja wa ndege wa Tan Hati Nhat katika mji
wa Chi Minh
Kesi ambayo imezuiwa kutokana na wito wa kidiplomasia hali
iliozua tumbo joto kuhusu msimmao mkali wa kisheria ambao nchi ya Vietnam huchukua
dhidi ya walanguzi wa dawa za Kulevya.
Nchi hiyo iliyo na sheria kali ambazo usipozingatia huenda makuu
yakakufika yakiwemo kunyongwa kwa mfano na baadhi ya sheria na masharti ambayo taifa hilo huweka kuzingatia ni kama.
Kifo dhidi ya usafirishaji wa dawa za Kulevya nchi hiyo huweza kuwa na sheria kali
dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya
duniani kote.Kulingana na sheria za nchi hiyo usafirishaji wa Gramu zaidi ya
600 za hiroini au zaidi ya kilo 2.5 huweza kusawasishwa na mtu Kunyongwa.
Katika Kesi ya Nduta mafisa wa Ukaguzi waliweza kubaini
kuwa zaidi ya kilo 2 za kokeini zilizokuwa
zimefichwa ndani ya begi lake
zilipatikana, licha ya yeye kusisitiza kuwa hakukuwa na ufahamu wa dawa hizo
kupatikana katika mkoba wake ila maamlaka ilimueleza kuwa mapuuza si utetezi na
sheria za Vietianamu dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya zingechukua mkondo wake
ipasavyo.
Uhalifu mwingine ni Kunyongwa kwa kupatikana kama umejidunga
dawa zizo hizo za kulenya mataifa mengi yanapozidi kuachana na sheria hiyo
taifa la Vietinamu lingali limeshikilia msimamo huo wa kunyonga watu .
Tangu mwaka wa 2013 taifa hilo limebadilisha mtindo
uliokuwepo wa kupigwa risasi na badala yake likakumbatia mtindo wa kunyonga,licha ya kuwepo kwa
shinikizo nyingi kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu kurai taifa hilo
kuuasi mtindo huo bado taifa la Vietinamu lingali limeshikilia mkondo huo
kuhusu kunyonga watu.
Kulingana na kujitetea kwake bi Nduta alisema kuwa kupitia
kwa mawakili wake kuwa mwanamume mmoja kwa Jina John ndiye aliyemwajiri ili ambebee mzigo huo ila Mahakama
ya Vietinamu ilisususia kuitikia ombi na rai za Bi Nduta na badala yake koti
ikaamuru anyongwe.
Taifa la Vietnamu huweza kusawazisha wale wote ambao ni Rai
wa taifa hilo au wageni kwa kuwanyonga pasi kuweka mipaka,katika miaka ya hivi
Karibuni raia wengi wameweza kunyongwa, hivo kesi ya bi Nduta ni baadhi ya Kesi
ambazo ziko huko vietnamu.
Hapa Kenya familai ya Bi Nduta iliweza kuomba taifa la Kenya
kuingilia kati kumwauni mwanao dhidi ya Kunyongwa .
Seneta wa Kisii aliweza kuiomba serikali ya Kenya kupitia kwa ubalozi wake Vietinamu
Kuingilia kati ili kumuani bi Nduta au
akitumikie kifungu chake hapa Kenya.
Wito kutoka kwa umma na Diplomasia kwa Jumla, makundi mbalimbali
yalirai Diplomasia ya Kenya kuingilia kati kubaini chanzo kikuu ni nini kilikusudiwa kuwa
raia wengi wanaopatikana huko ambao kipato chao ni haba huweza kunyanyashwa na
mabwenyenye na kupagazwa na kuzingiziwa dawa za kulevya.