Mbunge wa Gatundu Kusini Gathuka Gabriel Kagombe alisema kuwa aliyekuwa
Naibu wa Rais Rigathi Gachagua anajigamba kupita kiasi na ufuasi mkubwa kutoka Mlima
Kenya.
Akizungumza katika mahojiano na Kituo kimoja nchini
kinachotangaza kwa Lugha ya mama mnamo Machi 18,2025 Kagombe alisema kuwa
mazoea na tabia ya bwana Gachagua kujipiga kifua na kujigamba kutokana na uungwaji mkubwa wa eneo la Mlima Kenya ni wa
kupitiliza sana na kukanusha kuwa si kweli anavyojinadi.
Kulingana na usemi wa Bwana Kagombe alisema kuwa Bwana
Gachagua alijipa mamlaka ya kuzungumzia watu wa Mlima Kenya pasi kuchaguliwa na
Wazee wa Jamii ya Gikuyu hivyo yeye anatangaza ufalme wake binafsi.
‘’Bwana Gachagua anataka kushikilia msimamao kuwa nafasi
anayoishikilia ni ya manufaa ya Jamii ya
Gikuyu na akumbuke hiyo nafasi hajapewa na Wazee wa Gikuyu hivyo anajitanua na kupiga injili yake peke
yake kwa kujipandisha hadhi ya Kiwango cha kuwa msemaji wa jamii ambapo si hivyo’’Kagombe
alisema.
Bwana Gachagua siku ya Jumatatu Machi 17,2025 alisema kuwa
mchango wake katika kampeni za mwaka wa 2022 zilizaa matunda na zilikuwa za hali
ya juu kuwashawishii wananchi hadi ikafikia uamuzi wa yeye kuteuliwa kama Naibu
wa Rais .
Gachagua aliweza kueleza kwa kusema kuwa kutokana na
usemi wake mwema na kuwaongelesha raia vyema hadi kufikia kiwango cha kumwamini
na alipokuwa akiwaambia wananchi kuhusu mchakato wa uongozi ambao ulimpa uwezo
wa kuwa kiongozi wa pili katika taifa.
‘’Tangu mwanzo Rais Ruto alifahamu wazi kuwa mimi si kiongozi
wa’ Yes Sir’ lakini bado aliniteua kuwa naibu wake kutokana na ushawishi
niliokuwa nao kwa wananchi hadi kuweza kunikweza na kufanya mimi kuwa kiongozo
mkuu kiwango cha naibu wa Rais''.
Bwana Gachagua Katika mahojiano hayo aliweza kuzungumzia
uzinduzi wa Chama chake kipya akisema kuwa mipango yote ilikuwa sawa na kuwa hivi karibuni kitaweza kuzinduliwa ambapo dereva
atakuwa ni Gachagua Mwenyewe alisema.
‘’Watu wana uchu na ari ya kujua jina la chama chetu Pamoja
na nembo na rangi kwa Jumla katika Mwezi
wa tano hapo ndipo mbivu na mbichi
itabainika tutaweza kuwaondoa wanachama kutoka chama cha UDA na kujiunga na chama
chetu kipya’’ bwana Gachagua alisema.
‘’ Tungependa kuziomba Jamii zingine ziungane na sisi tutazipa
nafasi za uongozi katika serikali kufikia sasa viongozi wengine tayari wana vyeo
kwa hivyo tunaomba wale wengine waje upesi wapewe nafas katika meza ya
mazungumzo’’ bwana Gachagua alisema