Matiang'i amabaye alihudumu kama waziri wa elimu na waziri wa usalama wa ndani katika serikali iliyopita chini ya uongozi wa rais mustaafu Uhuru Kenyataa tayari ameonesha nia yake ya kuwania uongozi wa taifa.
Wazee hao wakizungumza wameeleza kwamba wao kama wazee wa Gusii pamoja na wenyeji wa eneo hilo kwa pamoja wanamwidhinisha Matiang'i anapotafuta nafasi ya kuwa rais.
"Sisi wazee wa Gusii pamoja na wenyeji tungependa kutangaza hadharani umoja wetu wa kumuunga mkono Dkt Fred Okeng'o Matiang'i anapowania ofisi kubwa kwa taifa. Kama kijana wa familia ya Gusii na ameteuliwa na watumishi wa Kenya ana historia ya kazi aliyofanya wakati wa rais Uhuru Kenyatta kwa wizari mbili ambazo alihudumu kwazo," wazee hao walisoma kauli yao.
Wazee hao pia walimutaja Matiang'i kama aliebadilisha mengi kwenye wizara ya teknoloja kwa wakati alipokuwa huko. Pia wakimpongeza kwa dhati kwa kazi ya kusifika alipohudumu kama waziri wa elimu. Wamemtaja kama aliyerejesha imani miongoni mwa mitihani ya kitaifa. pia wamemhongera kwa kuongoza kuleta tiba ya bure miongoni mwa wanafunzi na matumaini makubwa kwa vyuo vikuu.
"Kile ambacho kinajulikana sana ni wakati akiwa waziri wa elimu, alisafisha sana hasa kwenye mitihani ya kitaifa kwa kuleta imani kwenye mitihani hiyo kwa mamilioni ya wanafunzi. Hili lilifanyika kupitia kuweka sheria kali kwa usimamizi na wanafunizi iili kuzuia wizi wa mitihani," walieleza.
Vile vile wamemtaja Matiang'i kama waziri wa kujivunia wakati akiwa kwenye wizara ya usalama wa ndani.
"Kama waziri wa usalama wa ndani Dkt Matiang'i alihakikisha usalama wa taifa uko imara kwa muendelezo muzuri wa kazi ya serikali. Aliweka uwazi Kwenye wizara ambayo ni ya muhimu sana kwenye wizara za serikali," walisisitiza wazee hao.