Wizara ya kilimo yatarajiwa kuanza usambasaji wa magunia ya
mbolea zaidi ya milioni moja kwanzia leo
24 Machi,2025.
Kulingana na taarifa rasmi kutoka kwa Waziri wa
Kilimo Mutahi Kagwe aliweza kufafanua kwa kusema kuwa changamoto ambazo zilikuwepo
katika idara hiyo siku za hivi karibuni zilikuwa zimetatuliwa na hivyo muda mwafaka wa usambazaji wa mbolea ulikuwa umewadia.
‘’Ningependa kuwahakikishia wakulima kuwa changamoto zote
ambazo zilikuwa zimeikumba wizara ya kilimo tayari zimetatuliwa na kwa hivyo
kuanzia Jumatatu ya 24 Machi,2025 usambazaji wa mbolea utang’oa nanga bila
matatizo yoyote’’. Waziri alisema.
Kulingana na barua iliyoandikwa na wizara hiyo mnamo Machi
22,2025 iliweza pia kudadavua na kusisitiza kwa kina umuhimu wa kilimo pamoja
na wakulima kuweza kupata mbolea ili kuhakikisha kuwa wanaimarisha kilimo katika taifa letu ili
kuongeza mjazo wa chakula kingi nchini.
‘’Wizara ya kilimo na
mifugo ina furaha kusema kuwa kulingana na historia kubwa ambayo
imekuwepo katika wizara ya kilimo kwa wakulima kupokea mbolea ambayo ina ruzuku
kwa wakulima ambao walijisaji katika bodi ya wakulima wa kenya na udhibiti wa
usimamaizi wa kimawasiliano(Kenya integrated Agricultura lManagement
information system KIAMSI) kwa ajili ya
mvua nyingi watafaidi kwa sababu ya kuweza kuzalisha chakula kingi hivyo kuliepusha
taifa dhidi ya kuagiza chakula nje.
Wizara hiyo pia iliweza kuelezea kuwa kwa muda bodii ya
nafaka na mazao nchini(NCPB) ilihifadhi magunia ya mbolea zaidi ya 2.6m tangu Disemba 2024 na zaidi ya
mgunia 2.6 m yamesambazwa kwa ajili ya upanzi katika mvua za msimu mrefu.
Wizara pia iliweza kufafanua kwa kusema kuwa kutokana na hamu
kuu na hitaji la wakulima kutaka mbolea kwa wingi hio ni kuonyesha kuwa kama taifa
tutakuwa katika nafsi nzuri ya kujikimu katika kilimo siku za hivi karibuni.
Hata hivyo wizara pia ilisikitikia hali ya wakulima kufika
katika bodi ya nafaka na mazao kwa ajili ya kupokea mbolea yao ya ruzuku ila kulingana na hitilafu za kimitambo zoezi hilo halikufanikishwa
jinsi ilivyokusudiwa.
Serikali kupitia kwa Wizara hiyo ya kilmo na mifugo iliweza
kusema kuwa wanafanya jitihada na juhudi zote zimewekwa ili kuhakikisha
kuwa kila kitu kinaendeshwa jinsi kilivyoratibiwa.
Wizara iliweza kutangaza kwa kusema kuwa zaidi ya magunia
milioni moja yatatolewa kwa wakulima
katika matawi yote ya bodi ya nafaka na
mifugo ilioidhinishwa na kuwarai wakulima kuwa waangalifu kutokana na matapeli
wanaouza mbolea ghushi ambayo haijafikia viwango vinavyohitajika,wiraza ikisema
kuwa iko macho kuwaadhibisha matapeli hao kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria dhidi ya kumdhulumu mkulima.