logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Super Metro kuanza shughuli zake baada ya mahakama kuwapa idhini

Amri ya muda inatolewa kurejesha huduma za utekelezaji na uendeshaji wa magari Super Metro.

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri24 March 2025 - 12:13

Muhtasari


  • "Kampuni ina uhuru wa kuendelea na shughuli mara moja kwa kufuata sheria." barua ilisoma zaidi.
  • NTSA huku ikisimamisha operesheni ya PSV ilisema uamuzi huo ulikuwa kuhakikisha kampuni hiyo inatii hatua za usalama barabarani.

Super Metro Limitted Company
Kampuni ya magari ya Super Metro inatazamiwa kurejesha shughuli zake baada ya mahakama kuondoa kwa muda zuio lililowekwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama NTSA.

Bodi ya Rufaa ya Utoaji Leseni za Usafiri katika agizo lililotolewa Jumatatu, Machi 24, 2025, iliipa kampuni ya uchukuzi ya Super Metro kuanza kufanya kazi mara moja.

Amri ya muda inatolewa kurejesha huduma za  utekelezaji na uendeshaji wa walalamishi wa Machi 18, 2025, kusimamisha shughuli za kampuni ya Super Metro  kama waendeshaji wa PSV," agizo kwa mwenyekiti wa bodi Adrian Kamotho lilisomeka sehemu.

"Kampuni ina uhuru wa kuendelea na shughuli mara moja kwa kufuata sheria." barua ilisoma zaidi.

Kamotho pia aliamuru hati ipelekwe kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, mara moja. Shughuli za super metro zilisitishwa Alhamisi na NTSA.

NTSA huku ikisimamisha operesheni ya PSV ilisema uamuzi huo ulikuwa kuhakikisha kampuni hiyo inatii hatua za usalama barabarani.

Kusimamishwa kulianza Machi 20, 2025. "Hii ni kupitia kuarifu Umma kwamba Mamlaka imesimamisha leseni ya waendeshaji wa Super Metro Limited hadi Kampuni itii kikamilifu Kanuni za Magari ya Utumishi wa Umma, 2014 na masharti mengine yaliyowekwa," NTSA ilisema katika taarifa.

"Uamuzi huo ulilazimishwa na hitaji la kuhakikisha Kampuni sio tu inafuata sheria bali kwamba imeweka hatua za usalama kulinda maisha ya abiria wake na watumiaji wengine wa barabara."

NTSA ilidai kuwa kusimamishwa kazi kulifuatia ukiukaji mbalimbali wa wahudumu wa magari hayo, ikiwa ni pamoja na vyeti vya ukaguzi vilivyokwisha muda wake na leseni za huduma za barabarani, vyeti vya kudhibiti mwendo vilivyoisha muda wake, ukosefu wa rekodi za kudhibiti mwendo miongoni mwa mengine.

Mamlaka hiyo iliendelea kudai kuwa baadhi ya sifa za madereva hazikidhi sifa zinazohitajika pamoja na ukiukwaji wa kanuni za Uendeshaji wa Magari ya Watumishi wa Umma.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved