logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 25.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri25 March 2025 - 06:57

Muhtasari


  • Katika taarifa ya Jumatatu, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
  • Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nandi, Elgeyo Marakwet, Trans Nzoia, Kisumu, Kirinyaga, na Kiambu.

KPLC

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 25.

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Nandi, Elgeyo Marakwet, Trans Nzoia, Kisumu, Kirinyaga, na Kiambu.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya South C, Riverside Drive, na Waiyaki Way zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Kapsarur, Henry Koskei Secondary, Tinderet, Mbogo Valley, na Meteitei katika kaunti ya Nandi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Chesubet, Kibuga Centre, Kamoi, Kimwarer, na Muskut katika kaunti ya Elgeyo Marakwet zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya Kaplamai, ,Motosiet, Kachibora, Kapkarwa na State Lodge katika kaunti ya Trans Nzoia pia zitakosa umeme.

Sehemu za mji wa Kisumu katika kaunti ya Kisumu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Makutano, Munyaka, Gathigiriri, na Gitaraka katika kaunti ya Kirinyaga pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, maeneo ya Ikinu, Githiga, Gathanji, na Ngogoro Factory katika kaunti ya Kiambu pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved