Kenyatta ambaye alitawala Kenya kwa miaka kumi kama rais kupitia chama cha Jubilee amekuwa msitari wa mbele kwa muda mrefu akijitolea kuongoza mikutano ya kutafuta suluhisho katika mataifa yaliyokumbwa na vita.
Rais huyo wa zamani atakuwa miongoni mwa watu watano waliotikwa kwenye jukumu hilo muhimu baada ya mukutano uliowaleta pamoja viongozi wa nchi zilizoko chini ya mwavuli wa SADC na familia ya Afika Mashariki.
Viongozi wengine ambao wameteuliwa kushirikiana na Uhuru Kenyata ni rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, Kgalema Motlanthe wa Afrika kusini, Sahle-Work Zewde wa Misri na Catherine Samba-Panza wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Kwenye ripoti iliotolewa na mtandao wa raisi ilieleza kwamba walifanikisha kufanya mkutano usiku wa kuamukia leo 25 machi na wakafikiana kuwateua viongozi hao kuongoza mkutano wa kutafuta suluhisho la kudumu katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na migogoro ya kivita kwa muda mrefu.
"Jioni ya leo, kama mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, niliongoza pamoja na Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa wa Zimbabwe na mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi wa EAC-SADC juu ya kuongezeka kwa hali ya usalama Mashariki mwa DRC,' rais alisema kupitia mtandao wake.
Rais wa Kenya Dkt Wlilliam Ruto akitoa tangazo hilo kupitia mtandao wake rasmi wa Facebook alieeleza kwamba wamekubaliana kuhusu ripoti ya pamoja kati ya EAC - SADC kuhu mbinu zitakazo saidia kumaliza vita nchini DRC.
"Mkutano huo pia ulipitisha ripoti ya Mawaziri wa EAC-SADC ambayo inaelezea hatua za kusitisha mapigano, kusitisha uhasama na kuanzishwa kwa sekretarieti ya kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya mkutano wa pamoja," ujumbe ulisoma.