Shrika la ndege la Kenya KQ lilitangaza kupata faida ya shilingi bilioni 5.4 kutokana na huduma zake za usafiri.
Kulingana na chapisho lake rasmi kwenye mtandao wake wa X kampuni hiyo iliweza kutangaza kupata faida ya shilingi bilioni 5.4 baada ya kuenda hasara kwa takribani miaka 11 iliyopita.
Kampuni hiyo ambayo ina jumla ya ndege 35 ambazo hutua katika anga tofautitofauti za mataifa mbalimbali iliweza kurekodi faida hiyo kutokaana na usimamizi bora na utendakazi wa kufana.
Katika utendakazi wa mwaka wa 2024 kampuni hiyo iliweza kurekodi jumla ya shilinhi bilioni 5.4 ambacho ni kiasi sawa na dola za marekani 39.9 milioni, huku ikisafirisha abiria wengi waliosafiri kwa urefu wa miles 5.23 ambayo ni asilimia 4 huku ikibeba jumla ya tani zenye uzani wa elifu sabini na moja ambacho pia ni kiwango sawa na asilimia 25.
Kampuni hiyo vilevile iliweza kurekodi jumla ya matozo ya shiingi bilioni 188 ambacho ni kiwango sawa na dola bilioni 1.38 ambapo pia ni asilimia 6, kiwango cha huduma kwa jumla kikiwa shilingi bilioni 16.6 cha faida lilikuwa ni ongezeko la asilimia 58 na vilevile ilipata huduma za watumishi wa ndege katika shirika hilo ikipaanda hadi asilimia 75.2.
Kampuni hio kwa mara ya kuanza imerikodi faida hiyo baada ya kupata hasara kwa zaidi ya miaka 11 iliyopita itakumbukwa vyema kuwa wakati ambapo rais William Ruto alipochukua hatamu za uongozi aliweza kusema kuwa itakuwa ni wajibu wake kuhakikisha kuwa shirika hilo linatengeneza na kurekodi faida na kujisimammaia lenyewe.
Rais aliweza kusema hayo akilenga kuwa kutakuwa na uongozi maalum ambao utahakikisha kuwa kila kitu kinasimama wima na kuhakikisha kuwa pesa zinatumika vyema kulingana na idadi inayoohitajika.
Mnamo mwaka wa 2023 Kampuni hiyo iliwezakutangaza kupata hasara ya shilingi bilioni 22 lakini kulingana na juhudi za usimamizi kubadilishwa na vilevile kudhibiti matumizi ya pesa katika kampuni hiyo inakadiriwa kuwa kwa muda wa mwaka mmjoa imerekodi shilingi bilioni 28 ambapo ni faida ya shilingi bilion 5.4.