logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kenya yatuma mjumbe wa Amani Sudan Kusini kupatanisha pande kinzani

Rais William Ruto aliweza kuwasiliana na rais wa Sudan kusini Salvakir kuhusu tukio lililochangia Aliyekuwa Makamu wa Rais Riak kushikwa

image
na Evans Omoto

Yanayojiri28 March 2025 - 10:31

Muhtasari


  • Baada ya mazungumzo mapana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni na  waziri mkuu Abiy  wa Ethiopia  Rais aliweza kuafikia maamuzi ya kutuma wajumbe wa Amani katika Taifa hilo ili kuweza kubaini chanzo cha  tukio hilo na mbapo atajuzwa chanzo  cha mzozo huo.
  • Mnamo siku ya Jumanne Rais Ruto aliweza kufanya  mazungunmzo ya  amani na katibu mkuu wa  umoja wa kimataifa Bwana Marco Rubio  kuhusu hali  ya usalama katika taifa  la  Suadan kusini. 

Rais William Ruto aliwasiliana na rais wa Sudan  Kusini Salvakir kuhusu tukio lililochangia Aliyekuwa Makamu wa Rais Riak Machar kukamatwa.

Baada ya mazungumzo mapana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni na  waziri mkuu Abiy  wa Ethiopia  Rais aliweza kuafikia maamuzi ya kutuma wajumbe wa Amani katika Taifa hilo ili kuweza kubaini chanzo cha  tukio hilo na mbapo atajuzwa chanzo  cha mzozo huo.

'' Nimefanya mazungunmzo na rais  mwenzangu wa  Uganda Museveni na Waziri mkuu wa Ethiopia  Abiy na tumeafikiana kuwa nitatuma kikosi  cha  amani ambacho kitapiga msasa hali na kuniletea  ripot  kamili ya usalama huko ''. Rais Ruto alisema.

Mnamo siku ya Jumanne Rais Ruto aliweza kufanya  mazungunmzo ya  amani na katibu mkuu wa  umoja wa kimataifa Bwana Marco Rubio  kuhusu hali  ya usalama katika taifa  la  Suadan kusini, katika mazungumzo yao walijikita sana  katika  hali ya kuhakikisha kuwa amani ya  kudumu inajiri katika  mataifa hayo  mawili.

Mzozo katika taifa la Sudan kusini ulianza mnamo mwaka wa 2011 kati ya rais Salvakir  na Riek Machar ambapo kulikuwa na mzozo mkali sana uliosababisha mamia na  na maelifu ya  raia kuuawa na kupoteza makaazi zaidi ya  watu  40,000 waliweza kuuawa.

 Ulipofika mwaka wa 2018 mchakato wa upatanishi na kupata suluhu ya kudumu iliweza kuanzishwa ili kuafikia  hali ya amani katika taifa hilo na kuhakikisha kuwa viongozi hao wawili wanaletwa pamoja ambapo mpango  huo uliweza kufanikishwa na viongozi hao wakawa wanaishi kwa  amani na kwa upendo.

Hali ya kutoelewana ilianza tena hivi karibuni wakati ambapo ilisemekana kuwa Riek Machar aliweza kuuteka mji wa upper hill ambapo alionekana kushirikiana na wanajeshi Wazungu jambo ambalo lilisababisha wandani wa karibu wa Machar kuweza kukamatwa kwa kudhaniwa kuwa Machar alikuwa na njama fiche na wanajehi hao.

Jambo ambalo lilisababisha kufungiwa na jeshi katika maskani yake bila kutoka  alimaarufu 'house arrest' ili kuweza kufanya uchunguzi wa  kina na kubaini ukweli.

Taifa  la  Kenya limekuwa likishiriki katika mapatanisho ya amani katika mataifa mbalimbali na kuonyesha mchango mkubwa katika mataifa ya Afrika upatanishi wa  hivi punde ni kupata  suluhu ya  kudumu katika taifa la DRC ambalo limekuwa na mzozo wa muda mrefu na  waasi wa M23 vita ambavyo pia vimesababisha kufurushwa kwa wananchi na kuharibika kwa mali .

Kwa sasa Kenya itasubiri ripoti maalum itakayoletwa na  mjumbe  wa amani ili kubaini na kuelezea chanzo cha vita hivyo baada ya kuwepo kwa serikali ya pamoja ya amani kwa taifa mwaka wa 2018.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved