Aliyekuwa Jaji mkuu David Maraga alikubali wito wa vijana wa kizazi cha Gen Z kwa kuitikia wito wa kumtaka kuwania urais mwaka wa 2027.
Alizungumza akiwa katika Kaunti ya Migori Katika chuo kikuu cha Rongo baada ya kuwahutubia wanafunzi kuhusu maswala mabalimbali yanayofungamana na uongozi.
Jaji huyo wa Zamani aliweza kuelezea ari yake kuwa angependa tena kuongoza mhimili mwingine wa serikali kama alivyoongoza mahakamani kama jaja mkuu kwa miaka minne na miezi mitatu tangu mwaka wa 2016-2021.
''Nimehudumu mwanzoni kama Jaji mkuu katika jamuhuri ya Kenya kwa hivyo sioni kama kuna ubaya wowote mimi kuongoza mhimili mwingine wa serikali kwa kuwa ni jambo zuri tena lenye tija katika taifa na kwa wananchi" Maraga alisema.
Kulingana na mujibu wa maelezo yake Bwana Maraga alionyesha kuwa na uzoevu katika masuala ya uongozi hivyo alikuwa na imani fika iwapo angepewa fursa ya kuliongoza taifa bila shaka angetekeleza wajibu huo kwa kujitolea na kwa kuzingatia mwongozo wa katiba.
Hata hivyo aliweza kukosoa serikali iliyoko mamalakani kwa kuweza kuunda bajeti ya taifa ambayo ni fisadi na ambayo haioani na malengo wala mahitaji ambayo Wakenya wanatilia kipaumbele.
Alisuta wale ambao huunda na kukadiria bajeti ya taifa kwa kutotengea masuala muhimu pesa na kuangazia masuala ambayo mwananchi mlipa ushuru anakabiliwa nayo na badala yake bajeti huundwa kwa kuelekezea pesa nyingi kwa vitu ambavyo si vya muhimu sana kwa mawananchi mlipa ushuru.
''Kwa sasa ninafanya ushirikiano na washikadau mbalimbali ili kuweza kufanya tangazo rasmi kwa wananchi kuhusu msimamamo ambao nitakuwa nimeamua lakini kile ambacho ninashutumu kwa kusema kuwa ni tatizo kubwa nchini ni usfisadi na kukuwa na taasisi nchini ambazo ni fisadi''. Maraga .alisema.
Hata katika usanjari huo aliweza kuwarai wakenya kuishi kwa amani na kuwa katika mstari wa mbele kuwajibikia vitendo vyao na vilevile kuonyesha mifano miema katiaka uongozi wao.
David si wa kwanza kutoka jimbo la Kisii ambaye ameonyesha ari ya kuwania kiti cha urais nchini aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani Daktari Fred Matingi na Mwanaharakati Morara Kebaso ni miongoni mwa viongozi ambao wameonyesha ari ya kuwania kiti cha Urais mwaka wa 2027 hata hivyo bwana Maraga anakumbuwa na wengi kwa kuwa jaji wa kwanza kufutilia mbali matokeo ya urais ya mwaka wa 2017.