logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Shirikisho la Soka la Kenya latangaza tarehe ya mkutano

FKF imetoa taarifa ya kuelezea tarehe maalum ya kukutana ili kufanya mkutano wa mwaka.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri01 April 2025 - 11:44

Muhtasari


  • Katika barua iliyotumwa kwa matawi yote 48 simamaizi ya ligi mbalimbali  barua hiyo iliweza kuelezea na kutaja kila ligi ya timu jumuishi ili kuwa na ufahamu wa tarehe ya kuandaliwa kwa mkutano wa mwaka.
  • Halikadhalika klabu za kina dada zinazoshiriki ligi ya  daraja ya kwanza na mwakilishi wa wachezaji wa soka na msimamizi wa maslahi ya wachezaji.

Shrikisjho la soka nchini Kenya limetoa taarifa ya kuelezea tarahe maalum ya kukutana ili kufanya mkutano wa mwaka.

Katika barua iliyotumwa kwa matawi yote 48 ya kusimamia ligi mbalimbali, barua hiyo iliweza kuelezea na kutaja kila ligi ya timu jumuishi ili kuwa na ufahamu wa tarehe ya kuandaliwa kwa mkutano wa mwaka.

Barua hiyo ambayo ilitumwa kwa matawwi yote 48  mwanzo kwa kutaja klabu zote 18 zinazoshiriki katika ligi kuu nchini klabu 10 zinazoshiriki katika ligi pana ya taifa( National Super League) Klabu 10 zinazoshiriki ligi ya daraja ya kwanza na ya pili(Division 1 and 2) na  klabu tatu zinazoshiriki katika ligi ya kitaifa ya kinadada.

Halikadhalika klabu za kina dada zinazoshiriki ligi ya  daraja ya kwanza na mwakilishi wa wachezaji wa soka na msimamizi wa maslahi ya wachezaji.

Kulingana na kifungu nambari 29(2) cha sheria za shirikisho la soka nchini na katiba pamoja na afisi ya katibu mkuu ilitoa taarifa kwa wanachama wake kwa kusema kungekuwa na mkutano wa mwaka Mei 13,2025.

Tarehe 13,2025 barua ilieleza kuwa Mnamo tarehe hiyo bodi ya usimamizi ilipitisha kwa kauli moja kuwa mkutano wa pamoja wa mwaka ufanyike mnamo tarehe 31  Mei 2025 jijini Nairobi.

''Kwa hivyo barua ya notisi ndio hiyo inatolewa ya mkutano wa mwaka  kulingana na katiba ya shirikisho la soka nchini FKF'' sehemu ya barua ilieleza.

Agenda ya mkutano wa siku hiyo itatolewa mwezi mmoja kabla ya tarehe maalum ifike ambapo masuala kadhaa yatatolewa kwa ajili ya mkutano huo.

Barua hiyo pia iliweza kugusia na kuelezea wanachama kuwa wakufunzi na muungano wa marefari katika Jimbo la Nyamira na Homabay hawakufanya uchaguzi mkuu hivyo basi hawatawakiliswa katika mkutano huo ujao barua ilidadavua.

Barua hiyo iliweza kuandikwa na kutiwa sahihi  kutoka kwa katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Harold Ndege ambaye pia ni katibu mkuu mtendaji wa shirikisho la soka nchini FKF


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved