Maafisa wa kitengo cha ujasusi DCI maeneo ya Dandora kwa ushirikiano na maafisa wa kupambana na uhalifu waliwashika washukiwa wa wizi na ubakaji.
Washukiwa hao wawili walikamatwa kwa madai ya kutekaleza vitendo hivyo vya unyama mnamo Machi 11,2025.
Mwathiriwa mwanamke alikuwa alikuwa akiendesha gari katika barabara kuu ya Rua kuelekea Kangundo wakati ambapo gari lake lilipoteza mwelekeo na kukwama kando ya barabara.
Alipokuwa akifanya juhudi za kuhakikisha kuwa analiondoa gari lake kutoka mahali lilipokwama alifikiwa na wanaume wawili waliojifaanya kuwa wanataka kumsaidia kuondoa gari hilo kutoka mahali lilipokuwa limekwama ambapo pia walikuja watu wengine watano waliojifanya kuwa wasamaria wema.
Hatimaye nia yao ilibadilika na kumlazimisha mwenye gari kuingia katika buti ya gari na wakachukua usukani wa kuendesha gari na kuondoka.
Washukiwa hao waliweza kuendesha gari kutumia barabara ya Kangundo kupitia Mowlem na hatimaye kusimamia karibu na mto Nairobi kwa mbao- Dandora.
Walipofika hapo wliweza kumuondoa ndani ya gari huku wakimpiga na kumtendea unyama huo, hatimaye kutokana na kung'ang'ana mwathiriwa aliweza kuvutia mwendesha gari mmmoj aliyefika pale kutaka kujua kilichokuwa kikijiri.
Walipomwuona dereva yule akija kutaka kujua chanzo cha mvutano huo waliweza kuingia ndani ya gari na kuweza kutoroka.
Baada ya kumuokoa mwathiriwa aliweza kupelekwa katika kituo cha afya ili kupata matibabu ambapo tukio hilo liliweza kuripotiwa katika kituo cha polisi cha kwa Mbao.
Jambo la kusikitisha na kushangaza ni kuwa mwathiriwa aliweza kupoteza vitu vyake vyote alivyokuwa amenunua na bidhaa zake za kimsingi na hata kuibiwa pesa zake zote kutoka kwa Akaunti zake.
Mhasiriwa kwa sasa alikuwa katika hali ya unyanyapaa hio ni kutokana na dhuluma na hali ambayo alipitia wakati alipokuwa akikumbana na hali hio na washukiwa wale.
Aliweza kuwashukuru sana maafisa wa DCI kwa kufanya bidii na jitihada kuhakikisha kuwa wahusika wanakamatwa kutokana na makosa waliotenda.
Washukiwa hao waliweza kuwapeleka maafisa wa DCI katika mtaa wa Maringo Buruburu ambapo gari lililokuwa limeibwa liliweza kupatikana huku likiwa limeharibika.
Ushahidi mwingine ulioweza kupatikana kutoka kwa gari la mwathiriwa liliokuwa limeibiwa .
Washukiwa kwa sasa wapo kizuizini huku wakisubiri kufikishwa mahakamani huku polisi wakiendelea na uchunguzi kubaini na kuwakamata washukiwa wengine waliokuwa katika jitihada za kuwasaidia washukiwa hao kutekeleza wizi huo.