Rais Ruto mnamo Aprili 9,2025 alizindua kongamano la biashara duniani katika jiji kuu la Nairobi alimaarufu ''world chambers Federation African Summit''.
Ni kongamano ambalo lilikusudia kuyaleta pamoja zaidi ya mataifa 70 kutoka kote duniani kujadili masuala ya ushirikiano wa biashara duniani.
Kongamano hilo ambalo malengo yake makuu ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na uwekezaji mwema wa kuweza kuleta ufanisi wa biashara katika kujenga mazingira mazuri katika kuhakikisha kuwa wawekezaji wananufaika na kupata mazingira mema ya kuendeshea biashara.
Kwa kufanya hivyo ilikuwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wote wanajiendeleza kuweza kupata mtaji wa kiwango ambacho wanaweza kukimudu kwa kununua bidhaa katika mataifa mbalimbli jinsi wao wenyewe wapendavyo.
Rais pia aliweza kudokeza akisema kuwa kuweza kudumisha urafiki na ujirani mwema katika ulingo wa biashara bila shaka hapo utakuwa unakuza misingi na mifumo imara ambayo huweza kuleta ufanisi mkubwa katika kukuza biashara njema ndani ya nchi husika.
''Kwa kuweza kuweka masikio yetu katika hali ya kuwasikiliza wajasiriamali kupitia kwa taasisi kama zile za uhasibu na viwanda vya kitaifa kwa kufanya hivyo tunarahihisha wepesi wa kufanya kazi katika nchi yetu'' Rais aliweza kusema katika kongamano hilo.
Rais alikuwa ameandamana na waziri wa biashara na mikopo ya hazina ndogondogo kwa wafanya biashara nchini Wyckliff Oparanya ambapo muonekano wao waliweza kuhakiksha kuwa kongamamao hilo linakuwa ni la kufana sana.
Kongamano hilo liliweza kuwaleta pamoja washikadau mbalimbali katika sekta ya biashara kusudio na lengo kuu likiwa ni kuimarisha uchumi na biashara miongoni mwa wafanyabiashara katika viwango mbalimbali.
Kongamano hilo linakusudia kuwaleta pamoja viongozi kutoka matabaka mbalimbali,wawekezaji,wafanyabiashara na washikadau wa serikali kutoka mataifa mbalimbali ambapo lengo na kusudio kuu ni kuhakikisha kuwa biashara inastawi na kukuwa kote duniani.
Kenya kwa miaka mingi imekuwa mwenyeji wa hafla mbalimbali za kitaifa ili kuweza kuhakikisha kuwa mipango ya uwendelevu kuhusu masuala mbalimbali yanatekelezwa na kuwekwa katika viwango vya kuheshimika si biashara bali hata masuala ya usalama na hata makongamano ya kuhusu tabianchi.