logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Malala awahongera wanafunzi wa Butere Girls kwa kususia kuigiza 'Echoes of War'

Malala alielezea uamuzi wa wasichana hao kuwa ni tukio la kishujaa kwa wasichana hao.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri10 April 2025 - 12:21

Muhtasari


  • Malala alisema kuwa ni jambo lisilofaa kwa maafisa kuwakatalia wasichana haki yao ya kutumbuiza mbele ya hadhira.
  • Katibu Mkuu huyo wa zamani wa UDA aliwatia moyo wasichana hao kubaki na matumaini na ujasiri.

Mwandishi wa Tamthlia ya Echoes of war

Aliyekuwa Seneta wa Kakamega, Cleophas Malala, amewapongeza wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Butere baada ya kususia kucheza wa tamthilia yake Echoes of War.

Akizungumza kwa simu kutoka Kituo cha Polisi cha Eldama Ravine, Malala alielezea uamuzi wao kuwa ni tukio la kishujaa kwa wasichana hao.

Aliongeza kusema kuwa ni jambo lisilofaa kwa maafisa kuwakatalia wasichana haki yao ya kutumbuiza mbele ya hadhira.

“Ilkuwa ni tukio la kishujaa kwa wasichana hao kwa sababu wangeweza kutumbuiza bila ya hadhira, mapambo, mavazi, na waongozi wao. Hiyo ni kinyume na haki, na naamini maafisa wanapaswa kuwajibika kwa kuwanyima wanafunzi haki yao ya kutumbuiza katika shughuli ya kisanii,” Malala aliambia kituo kimoja cha redio.

Maneno yake yalifuatia ripoti kuwa wasichana walipanda jukwaani, wakiimba wimbo wa taifa kisha wakatoka, wakidai mkurugenzi wa tamthilia, ambaye ni Malala.

Wakati walipopata nafasi ya kuonyesha tamthilia hiyo, inadaiwa pia walikataa baadhi ya miundombinu muhimu iliyokuwa imetolewa kwa shule zingine ili kuboresha mchezo wao, kama vile mikrofoni, vifaa vya uigizaji na vifaa vingine.

Malala alikamatwa usiku wa Jumatano.

Katibu Mkuu huyo wa zamani wa UDA aliwatia moyo wasichana hao kubaki na matumaini na ujasiri.

Alisisitiza kuwa sasa wamekuwa sehemu ya historia ya Kenya na watazikumbukwa kama sehemu ya watu waliopigania uhuru wa Kenya.

“Ningependa kuwahimiza, wakusanye matumaini na ujasiri. Huu ni wakati mkubwa ambapo wanakuwa wachezaji wakubwa katika kusambaza taarifa muhimu kwa umma na kwa hivyo wanapaswa kuvaa uso wa ujasiri na kujua kuwa wameandikishwa katika historia kama watu waliopigania uhuru wa nchi hii.

Malala aliongeza kuwa anawahurumia wanafunzi wa Butere Girls kwa yale waliyopitia kwa sababu ya tamthilia hiyo.

“Sherehe ya drama imekuwepo kwa muda mrefu sana na tuna aina mbalimbali za mambo yanayoonyeshwa katika Sherehe ya Taifa ya Drama na ni bahati mbaya kwa maafisa kuwaonea vijana hawa ambao wanajaribu tu kuonyesha kile wanachoona kama mabo maovu katika jamii. Ningependa kuwaomba wote wanaohusika na sherehe ya drama kuwa na akili timamu; hii ni tamthilia tu, na haina uhusiano wowote na uchochezi au majina ya kudhalilisha,” aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved