Maafisa wa polisi Kutoka kituo cha polisi cha Narok waliwakamata washukiwa watatatu wa wizi siku ya Alhamisi.
Washukiwa hao watatu wa wizi walikamatwa kwa tuhuma za kutekeleza wizi pamoja na kusababisha vurumai katika mji mkuu wa Narok pamoja na viunga vyake.
Kukamatwa kwao kulitokana na wananchi kulalamikia kuhusu hali mbaya ya usalama katika kijiji cha Total Kaunti ya Narok.
Kwa kuweza kuzingatia na kufuatilia kwa karibu wito wa wananchi Maafisa wa polisi waliweza kuwakamta washukiwa watatu ambao walikisiwa kupatikana na vifaa vya nyumbani waliweza kupatikana na simu za rununu, vipakatalishi na mitungi ya gesi.
Katika vurumai hiyo mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Maasai mara wa mwaka wa tatu aliweza kujeruhiwa vibaya sana kabla ya wezi hao kutekeleza wizi na kuondoka.
Kutokana na juhudi za mchwa za maafisa wa polisi ambao walijaribu kufuatilia tukio hilo kwa upesi hadi wakaweza kuwakamata washukiwa hao watatu .
Maafisa wa usalama waliweza kupata visu vitatu vya Maasai kuashiria kuwa washukiwa hao walikuwa na nia mbaya ya kutaka kutekeleza maangamizi, waliweza kushikwa pia na kipakatalishi aina ya Lenovo, Simu saba,na mtungi wa gesi wa kilo sita.
Baada ya wa washukiwa hao kukamatwa waliweza kuwapeleka maafisa wa polisi katika maskani yao ambapo bidhaa zingine ziliweza kupatikana vifaaa vya kielektroniki,mtungi wa gesi,mita ya Kenya Power, na vifaa vingine vilivyoweza kupatikana na wenyewe,
Mpangaji aliyeweza kujeruhiwa aliweza kupelekwa katika hospitali ya chuo kikuu cha maasai mara kwa matibabu ambapo ilisemekana kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.
Washukiwa hao kwa sasa wako kizuizini wakisubiri kufikishwa kortini ila vifa ambavyo walipatikana navyo vimehifadhiwa kama ushahidi wa kutosha ili kuweza kushadidia kesi za hao washukiwa watakapofikishwa kortini.
Visa vya wizi vimekuwa vikiripotiwa kwa sana maeneo hayo huku wananchi wakiwa wameripoti kuhusiana na kupotea kwa bidhaa zao huku washukiwa wakiwa katika misako mikali ya kuwakamata.
Kwa hivyo inaashiria kuwa waliokaamatwa watakuwa sasa miongoni mwa wale wezi sugu ambao wamekuwa wakiwahangaisha wananchi na vilevile kuweza kuwaafikisha katika mahakama ili kujibu mashitaka ya wizi.