

Waziri mteule Geoffrey Ruku wa utumishi wa Umma alikuwa katika bunge la taifa kwa ajili ya kupigwa msasa.
Ruku ambaye alikuwa mbunge wa Mbeere Kasikazini aliteuliwa na rais kuweza kuhudumu katika nafasi ya waziri wa utumishi wa umma baada ya waziri aliyekuwepo Justine Muturi kusimamishwa kazi na rais.
Geoffrey Ruku alihitimu masomo yake katika chuo kikuu cha Nairobi kwa kusomea taaluma ya uhasibu mnamo mwaka wa 2008 na 2009.
Hatimaye aliweza kujiongezea elimu kwa kusomea taaluma ya uhusiano mwema katka nchi za kimataifa kama mwanadiplomasia mwaka wa 2003-2005.
Hatimaye mwaka wa 1998 hadi 2002 Ruku aliweza kusomea taaluma ya biashara na kupata shahada hiyo katika chuo kikuu cha Catholic.
Ruku ana tajiriba pana katika safari yake ya uongozi mnamo mwaka wa 2006 na 2009 kama balozi wa Kenya nchi ya Israel, mnamo mwaka wa 2010 hadi 2011 alikuwa afisa mkuu mtebdaji wa gesi ya Kaboni Afrika.
2015 na 2017 alikuwa afisa wa siiri katika kampuni ya maji na uwekezaji wa hela huku mwaka wa 2013 na 2015 kama mwanakandarAsi huru.
Mnamo mwaka wa 2017 na 2025 hadi kama mfanyabiashra na mshauri mkuu ambaye amekuwa kwa jukwa katika soko kuu.
Siku ya jumatatu ya tarehe 14 Aprili,2025 alikuwa mbele ya jopo la kumhoji ambapo aliweza kuelezea kwa kina kuhusu ufahamu wake kulingana na zao la miraa na mugoka ikikisudiwa kuwa kule alikotoka ndiko kitovu cha zao hilo.
Alikuwa anajibu swali ambalo mheshimiwa Baya alitaka aelezee bunge wakati ambapo alikuwa katika kamati hiyo ya kilimo akiwa mbunge ilibainika kuwa aliweza kuchochoea mabadiliko ambayo wabunge walitaka ufahamu ni kwa nini alifanya hivyo na vilevile wabunge walitaka kujua tofauti ya miraa na Mugoka.
Aliweza kusema kuwa miraa na Mogoka ni mimea ambayo inapatikana katika familia moja ya kisanzi ila tofauti ni kidogo kulingana na asili yake ya mwanzo .
Aliweza kukariri kwa kusema kuwa zao la miraa na mugoka lilikuwa likipandwa katika sehemu mbalimbali za taifa wala si sehemu moja tu jinsi ambavyo wengi walivyodadisi alisema kuwa miraa ilipandwa maeneo ya Meru, embu, Muranga, Machakosi na sehemu za Makueni.
Aliweza kusema kuwa miraa na mogaka ilikuwa na athari chanya za kiaya kwa watu kando na madai ya watu kuwa zao hilo ni baya kwa afya ya binadamu.