Shirika la kusambaza umeme nchini, Kenya Power, limetangaza kuwa baadhi ya maeneo katika kaunti saba nchini yatakumbwa na katizo la umeme siku ya Jumatano, kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kupitia taarifa iliyotolewa Jumanne jioni, shirika hilo limesema kuwa kukatwa kwa umeme kutasaidia kufanikisha shughuli za matengenezo ya mifumo ya kusambaza umeme ili kuboresha huduma kwa wateja.
Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Kajiado, Uasin Gishu, Vihiga, Embu, Nyeri na Kiambu.
Nairobi
Katika Kaunti ya Nairobi, maeneo kadhaa yataathirika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo hayo ni Mirema, barabara ya Lumumba, USIU, Thome 5, Safari Park View East, sehemu za TRM pamoja na wateja wa karibu.
Aidha, sehemu ya barabara ya Jogoo, soko la Burma, barabara inayoelekea Kaloleni, duka la Rikana, makazi ya serikali, hospitali ya Mary Immaculate, barabara ya Heshima na maeneo jirani pia yatapoteza umeme kwa muda huo.
Maeneo mengine yatakayoathirika ni Moi Education Centre, School of the Blind, uwanja wote wa ndege wa Wilson, Sunshine, T-Mall, Skyline Mall, vituo vya mafuta vya Shell na Rubis, kituo cha Bethel, Uhuru Gardens, Jonathan Ngeno, Maasai Court na Breeze East.
Kajiado
Katika Kaunti ya Kajiado, umeme utakatika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo yafuatayo: Barabara Mpya, Tom and Jerry, sehemu ya barabara ya Merisho, Rongai Exciting, barabara ya Kimani, Mayor Road, Maasai Lodge Road, Chuo Kikuu cha Nazarene, Tuala, Sigma Feeds, Rangau Olekasasi, Gataka, Kware na Emakoko.
Maeneo mengine ni Rimpa, Kandisi, SGR, Rangau, Kwa Muthaura, Metropolitan, Symurina na maeneo ya jirani.
Wateja walioko katika Maxwell University, Acacia East, Olesakunda, Magenche, Exciting, Kimandiro, Total, Laiser Hill, Nairobi Women’s Hospital, Fatima Hospital (Kaskazini na Kusini), sehemu za Kware, Tuskys, Kingdom Hall, Wama Hospital, mji wa Rongai, Sinai Hospital na maeneo ya karibu pia wataathirika.
Vilevile, umeme utakatwa katika maeneo ya Kanisani Road, Kwekwe, Kahuho, Philothea, Kiserian Primary, Kiserian Town, Ndirangu Road, Narumoru, Gategi, Picnic Site, Brook-Hust, Emasho, Sholinge, Farmers, NPC, Olorien, Birika, Ostrich Farm, Kipeto na Saithy Sai.
Uasin Gishu
Katika Kaunti ya Uasin Gishu, maeneo yatakayopoteza umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni ni Lower Mugunga, Majengo, Smokin Wanjala pamoja na wateja wa karibu.
Maeneo mengine ni Bishop Birech, Wonifour, Katuiyo, Sirwo, Cheroroget, Mogobich, Rot-Tuga na maeneo ya jirani.
Vihiga
Kaunti ya Vihiga itakumbwa na katizo
la umeme kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo
yatakayoathirika ni Solongo Polytechnic, sehemu za soko la Chavakali, sehemu za
Mbale Market, Hams Hotel, Road Park Hotel, kituo cha mafuta cha Rubis, kijiji
cha Madegwa na maeneo ya jirani.
Embu
Katika Embu, umeme utakatika kati ya saa tatu na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni katika maeneo yafuatayo: sehemu za soko la Kivwe, Muruatetu, Mbukori, Manyatta, TIVET, Makengi, Karingari, Nembure, Kevote, Makuria, Ngai Ndethia na maeneo jirani.
Nyeri
Maeneo kadhaa katika Nyeri yataathirika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Haya ni Ngandu, kiwanda cha Kiamaina, Kiawanduha, Thangathi, Giakomu, Unjiru, Grando Kago, shule ya sekondari ya Ichuga, Gathumbi, Unjiru PCEA, kiwanda cha Kiawarigi, Kiangurwe, Gachuiro, General China, Gathu-Ini, shule ya msingi ya Gathu-Ini, Kihuro, soko la Itiati, Kiamaucheru, Itiati Mukonye, soko la Gitunduti, Kianjuguma, Gikore, Kihuri, minara ya Safaricom na Airtel.
Kiambu
Katika Kiambu, maeneo yafuatayo yatapoteza umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni: Total Gatitu, hoteli ya Cravers, TIBS, nyumba ya maombi ya Vincentian, shule ya Mangu, shule ya Compuera, Ndarugu Coffee East, sehemu za Ngoingwa, THIWASCO, Albizzia na wateja wa karibu.
Maeneo mengine ni Kanunga, Ngegu, Torito, Kasphat, Ibonia, Kiamara, Kiratina, pamoja na maeneo ya Kinoo, Gichecheni, Baraniki na maeneo jirani.