Wizara ya afya ilipokea barua kutoka kwa afisi inatoa huduma za uhamishaji wa viungo vya mwili iliyoandikwa 20 Julai 2023 kwa madai ya uuzaji wa viungo vya mwili.
Barua hiyo iliweza kuelezea ongezeko kuu la uuzaji wa figo kwa taifa la Israel,Jamii iliweza kushuku pakubwa ongezeko la watu kujitolea kwa ajili ya kuuza viungo vyao huku likitilia shaka uwezekano wa kuvunjwa kwa sheria za afya nchini.
Kulikuwa na taarifa za kuaminika kuwa uuzaji wa viungo vya mwili hasa figo vilikuwa vimekithiri ambapo mfadhili mkuu wa zoezi hilo alikuwa anatoka Israel ambapo alikuwa anashirikiana na hospitali ya Mediheal Eldoret.
Kutokana na tetesi hiizo wizara iliweza kuanzisha uchunguzi wa haraka kwa kuunda jopo la uchunguzi lililoshirikisha timu ya kamati ya upelelezi na adhabu iliyowajumuisha wataaalamu kutoka kwa kitengo cha madili,idara ya uhamishaji wa viungo vya mwili,mwakilishi kutoka kwa idara ya utoaji wa damu, waakilishi kutoka kwa muungano wa kutetea maslahi ya madktari, wawakilishi kutoka kwa wizara ya Afya na wawakilishi kutoka kwa muungano wa madaktari wa Meno.
Jopo hilo lilianzisha kwa haraka utafiti wa haraka ili kubaini ukweli wa madai hayo yaliyokuwa yameenea kwa kiwango kikubwa kwanzia tarehe 5 hadi 8 Disemba 2023.
Majukumu ya jopo hilo yalikuwa ni kuhakikisha kuwa yanahakiki madai yaliyoibuliwa na shirika la ubadilishaji wa viungo, kutathimini jinsi ya kubadilisha viungo hivyo katika hospitali hizo katika hospitali na kupendekeza hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa baada ya uchunguzi kutamatika na ripoti ya matokeo kutolewa.
Jopo liliweza kutathimini na kutaja vitengo muhimu ambavyo lilipanga kuja kuvishughulikia kwa mfano kuendeleza utoaji wa figo na jinsi ya kutoa moja kwa moja, kupiga tathimini ya muendelezo huo katika hospitali ya Mediheal hasa upande wa kubadilishaji wa viungo.Kuhakikisha kuwa inahitimisha ripoti na hatimaye kutoa mapendekezo kwa wizara ya afya.
Kulingana na matokeo ya jopo ni kuwa ilibainika kuwa Hospitali ya Mediheal ilikuwa ni hospitali ambayo ilikuwa katika mji wa Eldoret na ambayo iko katika kiwango cha level 5 na ambayo iliidhinishwa kwanza kufanya operesheni kadhaaa za kuhamisha viungo vya mwili na ilikuwa ikifanya hivyo kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na ambapo jumla ya visa vya uhamishaaji wa viungo 372 vilikuwa vimetekelezwa.
ilibainika pia kuwa hospitali hiyo ilikuwa imefanya shughuli hiyo kwa zaidi ya mataifa matano afrika mashariki Kenya,uganda,Burundi, Ethiopia ,DRC, Somalia na na mataifa ya ulaya kama Australia, Israel, Japan, USA na UK.