Waziri wa Afya Aden Duale mnamo tarehe 23 Aprili, 2025 alikuwa na mkutano na viongozi pamoja na washikadau wa afya.
Ni mkutano ambao uliongozwa na waziri Duale akiwa pamoja na mkuu wa maafisa wa usafi wa matabibu Profesa Samweli Kang'ethe kujadili masuala muhimu ya afya pamoja na usalama chini ya mfumo wa afya kwa wote UHC.
Akirejelea kifungu 33(2) cha mwaka wa 2023 bima ya afya kwa wote waziri aliweza kusisitiza kuhusu ombi la kamati la kuweza kudumisha madili ,ushahidi uliopo na uwazi katika kupatiana vibali vya kuhudumu pamoja na kufanya ukaguzi maalim wa vifaa vya matumizi katika hosipitali mbalimbali.
Katika kutoa muongozo maalum Duale aliweza kuwelezea akisema kuwa kibali kisipewe kwa afisa yeyote wa afya ambaye amesomea katika kituo cha afya ambacho hakijaidhinishwa rasmi, Kukaguliwa, kupigwa msasa na kamati maalum ya afya kutoka kwa wizara ya afya.
Kwa kuweza kuzingatia hayo tutakuwa tunalinda viwango vyetu vya afya pamoja na mifumo yetu ya matibabu katika ngazi zote za hospitali za afya.
Kwa kuhakikisha uwajibikaji waziri aliweza kuamuru kamati iweze kuanzisha uchunguzi katika mifumo yote ya afya na iweze kutuma ripoti ya hospitali zote ambazo zimesajiliwa na wizara ya afya pia aliweza kusisitiza habari zote na rekodi zote za afya ziweze kuhifadhiwa kidijitali.
Aliweza kuamuru kwa kusema kuwa habari zote za hospitali ziweze kuwekwa katika mfumo wa afya wa kidijitali wa serikali ili kuweza kuepukika na kupotea kwa rekodi pamoja na kusaidia kuweka viwango vyema vya ukaguzi.
Vilevile waziri aliwahakikishia wanajopo kuwa wizara ilikuwa radhi kujitolea na kushirikiana na washikadau pamoja na kuendeleza kampeni ya bima ya matibabu ya Taifa care pamoja na mfumo wa maendelezo wa ajenda ya mabadiliko ya uchumi alimaarufu BETA.
Waliokuwepo katika mkutano huo ni Katibu mkuu katika wizara ya Afya Mary Muthoni,mkurugenzi mkuu katika wizara ya afya Daktari Patrick Amoth na kaimu mshikilizi wa wizara ya uchumi wa digitali Bwana Anthony Lenaiyara.