Mwanasiasa wa Kenya na mgombea wa urais mara mbili, Mwalimu Mohammed Abduba Dida, ameachiwa huru kutoka gereza la Marekani baada ya kutumikia sehemu ya kifungo chake.
Dida alihukumiwa kifungo cha miaka saba kwa kosa la kumfuatilia na kumtisha mke wake Mmarekani katika jimbo la Illinois, lakini aliachiwa mapema kwa masharti na kuondoka gerezani tarehe 3 Machi 2025 — miaka minne kabla ya tarehe yake rasmi ya kuachiliwa iliyopangwa kuwa Aprili 3, 2029.
Kuachiliwa mapema kwa masharti ni hatua ya kisheria inayomruhusu mfungwa kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo chake akiwa huru katika jamii lakini chini ya uangalizi maalum.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kituo cha Marekebisho cha Big Muddy, ambacho kilikuwa kinamhifadhi, Dida sasa atahusika katika shughuli za kijamii za kutoa msaada kama sehemu ya masharti ya kuachiliwa kwake.
Dida alikuwa chini ya uangalizi wa kifungo tangu tarehe 18 Novemba 2022, alipotiwa hatiani kwa kuvunja amri ya mahakama iliyokuwa ikimzuia kukaribia maeneo maalum yanayohusiana na mke wake.
Hati za mahakama zinaeleza kuwa alikiuka amri hiyo kwa kwenda kusali katika msikiti uliopo karibu na makazi ya mkewe. Ingawa alidai lengo lake lilikuwa ni ibada, mahakama iliona kuwa uwepo wake mahali hapo ulikuwa ukiukaji wa sheria kwa kuwa mkewe pia huhudhuria msikiti huo mara kwa mara.
“Alikuwa anaenda tu kusali msikitini, hakujua kama msikiti huo ulikuwa ndani ya eneo alilokatazwa. Mama Lila naye husali hapo,” alisema jamaa mmoja wa familia.
Familia ya Dida inasema tukio hilo lilitokana na bahati mbaya, na sasa inaiomba serikali ya Kenya imsaidie kupitia msaada wa kisheria na kidiplomasia.
Kabla ya kuhamishiwa Big Muddy
Correctional Facility, Dida alishikiliwa kwa muda katika kituo cha Southwestern
Correctional Center