KWAHERI LUIZ

David Luiz apungia Arsenal kwaheri

Difenda David Luiz amewaaga mashabiki na wachezaji wenzake kwaheri baada ya kushiriki mazoezi yake ya mwisho na klabu ya Arsenal

Muhtasari

•Difenda David Luiz amewaaga mashabiki na wachezaji wenzake kwaheri huku baada ya kushiriki mazoezi yake ya mwisho na klabu ya Arsenal

David Luiz
David Luiz
Image: Hisani

Difenda wa timu ya Arsenali David Luiz amewaaga mashabiki na wachezaji wenzake kwaheri.

Hii ni kutokana ya mkataba wake na klabu hiyo ya London kutarajiwa kuisha mwisho wa msimu huu. Luiz alikuwa na mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya gunners.

Raia huyo wa Brazil alijiunga na klabu ya Gunners mwakani 2019 akitokea klabu hasidi ya Chelsea.

Siku ya Jumanne, klabu ya Arsenali ilitangaza kuwa ilikubaliana kutompa mchezaji huyo wa miaka 34 mkataba mwingine huku kocha mkuu Mikel Arteta akimsifia sana Luiz.

"Amesaidia sana, ni mtu tunayempenda na kumthamini sana kwa hivyo nasema tu asante na kumtakia kila la heri katika sura yake ijayo"  Arteta alisema.

Siku ya Jumamosi Luiz alishiriki mazoezi yake ya mwisho na klabu hiyo ya Arsenal huku akiwaaga wachezaji na mashabiki kwaheri na kuwashukuru kwa ushirikiano.

Luiz ameendelea kupokea jumbe za kheri njema kutoka kwa mashabiki na wachezaji mbalimbali.