Klabu ya Real Madrid imemsajili tena meneja Carlo Anceloti kwa kipindi cha misimu mitatu.
Meneja huyo wa miaka 61, mzaliwa wa Italia alihudumu tena kama kocha wa Real Madrid kati ya mwaka wa 2013 na 2015 huku akisaidia klabu hiyo kushinda kombe la mabingwa Ulaya mara moja.
Kurudi kwa kocha huyo kulitangazwa siku ya Jumanne na mabingwa hao wa mara 34 wa kombe la Laliga.
Ancelotti alikuwa kocha wa klabu ya Everton ya Uingereza msimu uliotamatika na alisaidia klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya kumi ikizoa pointi 56.
Official Announcement: Ancelotti.#RealMadrid | #WelcomeBackAncelotti
— Real Madrid C.F. 🇬🇧🇺🇸 (@realmadriden) June 1, 2021
Kando ya Real Madrid na Everton, Ancelotti amewahi kuwa mkufunzi katika klabu zingine tajika kama Juventus, Chelsea, Paris Saint-Germain(PSG), Bayern Munich, Napoli na AC Milan.
Ancelloti atakuwa anamridhi Zinedine Zidane ambaye aliondoka kwenye klabu hiyo msimu wa 2020/2021 ulipotamatika.
Klabu hiyo ilimaliza katika nafasi ya pili na pointi 84 msimu uliopita.
Ancelotti atazinduliwa rasmi katika uwanja wa Alfredo di Stefano siku ya Jumatano